BMT NA BMTZ YAAHIMIZWA KUIMARISHA USHIRIKIANO ILI KUINUA MICHEZO NCHINI.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Baraza la Michezo la Zanzibar  (BMTZ  yameshauriwa  kuimarisha ushirikiano ili kuinua sekta ya michezo nchini.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Zanzibar Mhe.  Rashid Ally Juma wakati  Kamati ya  maendeleo  ya Wanawake  ya  habari na Utalii ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar  ilipotembelea  BMT kujifunza mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Baraza hilo katika masuala ya michezo.

“Tanzania ni moja tuwe na ushirikiano mwema na mfumo  mmoja wa kuendesha michezo,” alisema Waziri.

20170419_093944
Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed kiganja akiwaelezea wajumbe kutoka Baraza la Wawakilishi baadhi ya miundombinu ya Uwanja wa Taifa kushoto kwake mwenye suti ni Waziri mwenye dhamana ya michezo Mhe. Rashid Ally Juma na Ujumbe wake.

Aliendelea kuwa, amefurahishwa na  uwazi ulioonyeshwa na watendaiji wa Baraza pamoja na Wizara kwa ujumla wake kuhusu uendeshaji wa michezo kwa Tanzania Bara.

Aidha,  Mhe. Waziri alisisitiza kuimarishwa kwa vitu vitatu katika Mabaraza hayo ili michezo iweze kuleta maendeleo zaidi, ikiwemo mawasiliano, ushirikiano na kuimarisha muungano wetu.

Awali Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi alitoa taarifa ya tangu kuanzishwa kwa  BMT pamoja na majukumu yake hadi sasa.

Aidha, Bw. Malinzi kwa niaba ya BMT ametoa shukrani kwa Kamati hiyo kuona umuhimu wa kufanya ziara hiyo  ambapo ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa BMTZ ili kuendeleza nchi yetu kupitia sekta ya Michezo ili kufikia uchumi wa kati.

32 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/04/19/bmt-na-bmtz-yaahimizwa-kuimarisha-ushirikiano-ili-kuinua-michezo-nchini/">
RSS