BMT LAANDAA SEMINA ELEKEZI YA UMISSETA

Baraza  la Michezo la Taifa (BMT)  kwa  kushirikiana na Kampuni ya  Vinywaji ya Coca cola wameandaa semina elekezi  ya maandalizi ya michezo kwa shule za Secondary (UMISETA) inayotarajiwa kufanyika tarehe 21 Aprili kuanzia saa 3:00 Asubuhi katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

Mgeni rasmi katika semina hiyo anatarijiwa kuwa Naibu Waziri Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Mhe.Suleiman Jafo.

Semina hiyo itahusisha Maafisa michezo  pamoja na Maafisa Elimu wa Mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani  ambapo watapewa maelekezo kuhusu mashindano hayo ya UMISSETA mwaka huu 2017 yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza.

Aidha, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  Bw. Mohamed  Kiganja  ametoa wito kwa  wahusika kuhakikisha wanafika  kwa wakati katika Semina hiyo ili michezo hiyo mwaka huu ifanyike kwa ufanisi na weledi mkubwa.

 

18 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/04/20/bmt-laandaa-semina-elekezi-ya-umisseta/">
RSS