SEMINA KWA AJILI YA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA (UMISSETA) YAFANYIKA MJINI DODOMA

21 Aprili, 2017

Semina maalumu kwa ajili ya kutoa maelekezo juu ya mashindano ya michezo kwa shule za sekondari (UMISSETA) yafanyika mjini Dodoma.

Semina hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya vinywaji nchini Coca Cola pamoja na Baraza la michezo la Taifa (BMT) likishirikiana  na ofisi ya Raisi Tamisemi imefanyika mwishoni mwa wiki tarehe 21 Aprili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

jofu
Naibu Waziri Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mh Suleiman Jaffo akifungua semina elekezi kwa ajili ya mashindano ya michezo kwa shule za sekondari (UMISSETA) kwa mwaka 2017.

Semina hiyo ilifunguliwa na Naibu Waziri ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) Mh.Suleiman Jafo akiwa mgeni rasmi na kuhitimishwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Annastazia Wambura.

Semina hiyo imeandaliwa ili kuwakumbusha Maafisa Michezo wa Mikoa yote pamoja na Walimu wa Michezo mambo muhimu ya kuziangatia kipindi cha mashindano ya michezo kwa shule za sekondari (UMISSETA) pamoja na kuwapongeza kwa mchango wao mkubwa wanaotoa katika kuendeleza Michezo nchini.

Msimamizi wa Copa Coca Cola Miss. Pamela Lugenye akitoa maelekezo jinsi kampuni hiyo  itakavyoshiriki katika kufanikisha mashindano ya  ( UMISSETA) kwa mwaka 2017.
Msimamizi wa Copa Coca Cola Miss. Pamela Lugenye akitoa maelekezo jinsi kampuni hiyo itakavyoshiriki katika kufanikisha mashindano ya ( UMISSETA) kwa mwaka 2017.

Kampuni ya vinywaji Coca cola ikiwa  kama mdau mkubwa wa michezo yatoa maelekezo ya jinsi itakavyoshiriki mwaka huu katika kufanikisha  mashindano ya UMISSETA.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa tarehe 28 Aprili mjini Dodoma ambapo Kampuni ya Coca Cola  imeahidi kuhusika na ugawaji wa vifaa vya michezo kwa shule zote za sekondari Tanzania, kuzamini vinywaji pamoja na maji ,chakula, waamuzi wa michezo, uzinduzi wa mashindano, pamoja na utoaji wa zawadi kwa washindi wote kuanzia ngazi  ya Mkoa mpaka Taifa.

 

Awali ya hayo Naibu Waziri Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mh. Suleiman Jafo aliwasihi Maafisa michezo wa Mikoa yote kusimamia maendeleo ya michezo  katika mikoa yao pia awaagiza Maafisa Elimu wa mikoa kuhakikisha shule zote  za michezo nchini zina walimu wa michezo wa kutosha.Mh Suleiman Jafo aliyasema hayo katika hotuba yake ya kufungua semina elekezi ya UMISSETA mjini Dodoma.

 

Pia, Mh.Naibu Waziri aliipongeza kampuni ya vinywaji Coca cola kwa mchango wao mkubwa katika kuendeleza michezo nchini na kuwaomba mashirika mengine kuiga mfano huo na kujitokeza kwa wingi kudhamini michezo Nchini.

Nae Naibu Waziri wa Habari,Sanaa ,Utamaduni na Michezo Mh.Annastazia Wambura ahimiza vijana kuzingatia maadili mema ikiwa na pamoja na kupinga matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Naibu Waziri wa Habari sanaa,utamaduni na michezo mh. Annastazia Wambura akihimiza vijana juu ya matumizi mabya ya dawa za kuongeza nguvu.
Naibu Waziri wa Habari sanaa,utamaduni na michezo mh. Annastazia Wambura akihimiza vijana juu ya matumizi mabya ya dawa za kuongeza nguvu.

Awaomba maafisa michezo na walimu wa michezo kuendelea kuwahimiza vijana kua utumiaji wa dawa izo za kuongeza nguvu ni kosa kubwa katika michezo.

wamburambele

Aidha Baraza la Michezo la Taifa , kampuni ya vinywaji Coca Cola pamoja na Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) yaahidi kushirikiana kuendeleza michezo nchini pamoja na kuhakikisha mashindano ya michezo kwa shule za sekondari (UMISSETA) yanafanyika kwa ufanisi mkubwa kwa mwaka 2017.

wamburapamoja
Naibu Waziri wa Habari sanaa,utamaduni na michezo mh. Annastazia Wambura katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, Wawakilishi toka Cocacola,mwakilishi toka Zanzibar,Maafisa Michezo wa Mikoa,Maafisa Elimu Mkoa ,na Walimu wa Michezo.

 

52 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/04/21/semina-kwa-ajili-ya-maandalizi-ya-mashindano-ya-umisseta-yafanyika-mjini-dodoma/">
RSS