CHAMA CHA MAGARI TANZANIA CHA HITIMISHA MAFUNZO YAKE YA USALAMA BARABARANI

24 Aprili, 2017

Chama cha magari Tanzania (AAT) yahitimisha mafunzo ya usalama barabarani  katika ukumbi wa shule ya Al-Haramain. Mafunzo hayo yametolewa ndani ya takribani shule 51 zikiwemo za chekechea msingi,sekondari,pamoja na vyuo vikuu.

1.Kamanda wa Jeshi la Usalama Barabarani Mohamedi R.Mpinga akitoa hotuba fupi katika maadhimisho ya mradi wa Usalama Barabarani
Kamanda wa Jeshi la Usalama Barabarani Mohamedi R.Mpinga akitoa hotuba fupi katika maadhimisho ya mradi wa Usalama Barabarani

Mgeni rasmi katika khafla hiyo alikua kamanda Wa Jeshi la Usalama Barabarani  Mohamed Mpinga  na wageni wengine ambao ni katibu mkuu wa baraza la Michezo la Taifa Mohamedi kiganja, Mwenyekiti wa AAT Nizari Jivani,katibu mtendaji wa AAT ndugu Yusuph Ghor,pamoja na mwalimu mkuu wa shule ya Al-Haramain.

kamada na katbu
4. Katibu mkuu baraza la Michezo la Taifa akikabidhi cheti kwa kamanda wa Jeshi la Usalama Barabarani.

Mafunzo hayo yametolewa na chama cha magari Tanzania (AAT) pamoja na Federation de Automobile international de Automobile(FIA) kwa kushirikiana na Baraza la Usalama la Taifa,baada  ya kuona ajali nyingi zinatokea kutokana na watoto kukosa elimu ya usalama barabarani.

5.Wanafunzi na walimu walioshiriki mafunzo ya Usalama Barabarani wakisikiliza hotuba ya Kamanda wa Jeshi la Usalama Barabarani
5. Wanafunzi na walimu walioshiriki mafunzo ya Usalama Barabarani wakisikiliza hotuba ya Kamanda wa Jeshi la Usalama Barabarani

Mafunzo hayo yalianza rasmi tarehe 10 Februali na kuhitimishwa tarehe 28 Aprili ambapo shule zilizo husika pamoja na wanafunzi waliohitimu wapewa vifaa mbalimbali vya kuwawezesha kutoa elimu hiyo kwa mashule na wanafunzi wengine.

3.Katibu mkuu mtendaji chama cha magari (AAT) ndugu Yusuph A. Ghor akipokea cheti cha ushiriki ya mradi wa Usalama Barabarani.
3. Katibu mkuu mtendaji chama cha magari (AAT) ndugu Yusuph A. Ghor akipokea cheti cha ushiriki ya mradi wa Usalama Barabarani.

Kamanda Mohamed Mpinga  awashukuru FIA  international, Chama cha Magari (AAT) na Michelin International kwa kuanzisha mradi wa mafunzo ya usalama barabarani na kufanya majaribio katika mkoa wa Dar es salaam.

Kamanda Mpinga apendekeza shule zianzishe  vikundi vya usalama barabarani  ambavyo vitasaidia  watoto mashuleni  kujenga kizazi chenye uelewa wa  Usalama Barabarani.

Nae Katibu Mkuu  Baraza la Michezo la Taifa ndugu Mohamed kiganja amshukuru kamanda Mpinga pamoja na makamanda wake wasaidizi kwa kazi ngumu waliyo ifanya ya kupunguza ajali Barabarani.

Katibu mkuu wa baraza la Michezo la Taifa akizungumza maneno        machache katika maadhimisho ya mradi wa Usalama Barabarani.
Katibu mkuu wa baraza la Michezo la Taifa akizungumza maneno machache katika maadhimisho ya mradi wa Usalama Barabarani.

Hafla hiyo ili itimishwa kwa ugawaji wa Vyeti kwa shule mbalimbali,wanafunzi,wafanyakazi wa Chama cha magari Tanzania , kikosi cha Trafiki pamoja na wafanyakazi mbali mbali waloiohusika katika kufanikisha mradi huo wa Usalama Barabarani.

walimu1

 

81 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/04/24/chama-cha-magari-tanzania-cha-hitimisha-mafunzo-yake-ya-usalama-barabarani/">
RSS