TAASISI YA HAMILTON AQUATICS YADHAMIRIA KUENDELEZA MCHEZO WA KUOGELEA NCHINI TANZANIA.

3 May 2017

Taasisi ya Hamilton Aquatics chini ya  Mkurugenzi Mkuu Chris Tidey na Afisa Mwendeshaji Mkuu Pippa Clark waleta mradi wa kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini.

Taasisi hiyo ikiambatana na Klabu ya kuogelea Dar es salaam(Dar swimming Club) chini ya Katibu Mkuu wake Inviolata Itatiro,  Meneja wake wa mradi Marry yakutana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la taifa (BMT) Dioniz Malinzi kuongelea mradi huo, mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Baraza ,Taifa jijini Dar es salaam

Hamilton Aquatics yaeleza juu ya  malengo yake ya kuendeleza mchezo wa kuogelea kwa kushirikiana na mashule mbali mbali kuanzia msingi mpaka vyuo pamoja na wazazi Tanzania. Taasisi hiyo inalenga kuanza  kutoa elimu ya kuogelea kwa watoto kuanzia miezi mitatu hadi tisa mpaka ngazi ya juu ya watu wazima.

20170503_103404
Katibu mkuu wa klabu ya kuogelea Dar es salaam Inviolata itatiro akitoa mawazo yake juu ya mradi wa Taasisi ya Hamilton Aquatics.

Malengo hayo wanategemea kuyatimiza kwa kujenga mabwawa yakuogelea kuanzia ngazi ya kufundishia mpaka ngazi ya mashindano ya kitaifa, kutoa walimu waliofudhu katika fani ya kuogelea na kutoa elimu bora ya kuogelea nchini.

Mradi huo unategemewa kuanza mkoani Dar es salaam na baadae kusambaa katika mikoa mingine ya Tanzania. Lengo la mradi huo ni kujenga kizazi chenye elimu ya kuogelea, kizazi chenye afya njema, kusambaza elimu ya usalama majini na kutengeneza watoto na vijana wenye  vipaji watakao iwakilisha Tanzania vyema katika ngazi ya Kimataifa.

Hamilton Aquatics inalenga kutoa elimu ya kuogelea kwa jamii nzima ya Watanzania bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia kwenye kipato, umri ,uwezo, rangi na tofauti nyinginezo.

Mweyekiti wa Baraza la Michezo naye alitoa ushauri wake kwa taasisi hyo jinsi ambavyo inaweza kuanza mradi huo, ambapo alishauri kwanza waanze kidogo kidogo kwa kujenga mabwawa machache ya kuogelea ambayo wataweza kuyamudu kwa wakati huu na pia walenge maeneo ambayo ni binafsi ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huo.

Taasisi hiyo ambayo ilisha fanya mradi kama huo kwa klabu ya kuogelea Dar es salaam (Dar swimming club) kwa muda wa miaka miwili na kuleta manufaa makubwa inategemea kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya mchezo wa kuogelea na elimu ya usalama majini nchini Tanzania.

 

77 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/05/03/taasisi-ya-hamilton-aquatics-yadhamiria-kuendeleza-mchezo-wa-kuogelea-nchini-tanzania/">
RSS