KAMPUNI YA SPORTS PESA YAKABIZI MSAADA WA HUNDI TSH. MIL 50 KWA WAZIRI DKT MWAKYEMBE KWA AJILI YA SERENGETI BOYS

11 May 2017

Waziri wa Habari  Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Harrison Mwakyembe amepokea Hundi ya shilling milioni 50 kutoka kampuni ya Sportpesa maalumu kwa kusaidia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17(Serengeti boys).

Waziri Mwakyembe akitoa  maneno ya shukrani baada ya kupokea hundi ya  shilingi million 50 kutoka kampuni ya sportpesa.(kushoto) mwenyekiti wa Baraza la Michezo la taifa Bw.Dioniz Malinzi.(kulia) Bw.Tarimba Abbas
Waziri Mwakyembe akitoa maneno ya shukrani baada ya kupokea hundi ya shilingi million 50 kutoka kampuni ya sportpesa.(kushoto) mwenyekiti wa Baraza la Michezo la taifa Bw.Dioniz Malinzi.(kulia) Bw.Tarimba Abbas

Utoaji wa hundi hiyo ni utekelezaji wa ahadi ambayo waliitoa katika uzinduzi wa huduma yao ya sportpesa tarehe 9 mei Katika ukumbi wa Kilimanjaro hotel ambapo Mh. Harrison Mwakyembe alikua ni mgeni rasmi.

Waziri Mwakyembe  ameishukuru kampuni hiyo ya Sportpesa kwa mchango wao na ameahidi kua serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa Michezo kuhakikisha sekta hiyo inafanya vizuri mpaka kwenye ngazi ya kimataifa.

Aidha awahimiza wadau wengine ambao walitoa ahadi ya kuisaidia timu hiyo ya Serengeti boys kutimiza ahadi zao ili kufanikisha ushiriki wa timu hiyo katika michuano itakayo fanyika nchini Gaboni ndani ya mwezi huu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa utawala na utekelezaji  kutoka kampuni ya Sportpesa Bw.Tarimba Abbas amesema  kua ameshatekeleza ahadi ambayo ilitolewa na kampuni hiyo.

IMG_4603

 

76 total views, 3 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/05/11/kampuni-ya-sports-pesa-yakabizi-msaada-wa-hundi-tsh-mil-50-kwa-waziri-dkt-mwakyembe-kwa-ajili-ya-serengeti-boys/">
RSS