BMT YAKABIDHI BENDERA KWA TIMU YA FCVITO.

Timu ya watoto ndani ya miaka tisa mpaka kumi na moja (11)  kutoka lindi FCVITO iliyopo chini ya mpango wa maendeleo  Michezo nchini (SDA) yakabidhiwa bendera leo Julai 4, 2017 na Katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamedi Kiganja  katika  ukumbi wa ubalozi wa Finiland, jijini Dar es salaam. Timu hiyo itaanza safari yake julai 5 2017 kuelekea Helsinki nchini  Finland kwa ajili ya michuano ya mpira wa miguu ya vijana maarufu kama Helsinki Cup.

20170704_102946
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohamedi Kiganja akizungumza maneno machache na vijana wa timu ya FCvito katika ghafla ya kuwakabidhi bendera ndani ya ukumbi wa ubalozi wa Finland jijini Dar es salaam.

Aidha katibu mkuu  ameushukuru ubalozi wa Finiland pamoja na mpango wa maendeleo ya Michezo nchini (SDA)  kwa kutoa mchango wao kufanikisha safari ya timu hiyo, pia amewashukuru wazazi kwa kuwa na imani na vipaji vya watoto wao na kuwaruhusu kushiriki michuano hiyo.

20170704_095511

Aliongeza kwa kusema michezo  haiui Elimu bali inaleta hamasa kwa vijana kwenda shule na kuwafanya wawe mahiri darasani kwa hiyo mpango wa kuendeleza michezo nchini (SIDA) ni wa muhimu kwa watoto wanaondeleza vipaji vyao katika michezo.

 

 

20170704_103815
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo La Taifa akikabidhi bendera kwa timu ya vijana ya FCvito,katika ukumbi wa ubalozi wa Finland jijini Dar es Salaam.

36 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/07/04/bmt-yakabidhi-bendera-kwa-timu-ya-fcvito/">
RSS