TIMU YA RIADHA YA UMRI CHINI YA MIAKA 17 YAREJEE NCHINI NA USHINDI

28 JULY, 2017

Timu ya riadha ya vijana chini ya miaka 17 imeleta heshima kwa Watanzania baada ya kurejea nyumbani na medali ya shaba aliyoshinda kijana Francis Damasi katika mbio za mita 3000 kwenye mashindano ya Jumiya ya Madola yaliyomalizika hivi karibuni huko nchini India.

katbu1
Timu hiyo imerejea leo na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere huku akieleza kufurahishwa na matokeo hayo mazuri waliyopata wanariadha hao ambao wameitangaza vyema Tanzania.
“Serikali tunawapongeza sana kwa kuitangaza nchi yetu lakini pia kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu katika mashindano haya nawaahidi nitaendelea kushirikiana na uongozi na wadau wa riadha nchini ili tufike mbali zaidi” Alisema Prof. Elisante Ole Gabriel.

mshind1
Kijana Francis Damian aliyepata medali ya dhahabu.

Kwa upande wake Mkimbiaji wa zamani na Mdau mkubwa wa riadha nchini Bw. Filbert Bayi amesema kuwa mchezo wa riadha kwa sasa ni mchezo ambao umeitangaza Tanzania kwa kiasi kikubwa kutokana na kushiriki mashindano mengi ya Kimataifa hivyo ni vyema wadau kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika mchezo huo ambao umeendelea kuiletea heshima Tanzania.

filbertbay
Katibu mkuu wa kamisheni ya olimpiki Tanzania(TOC)Filbert Bayi akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo picha mara baada ya mapokezi ya timu.

“Riadha imeitangaza Tanzania na itaendelea kuitangaza hivyo wadau wanapaswa kuitumia fursa hii kwa kuwekeza katika mchezo huu ili ufike mbali,kila mtu katika eneo lake aone fursa hii na aitumie kwa manufaa ya kizazi hiki na kitakachokuja” Alisema Bw. Bayi.
Naye Kijana Francis Damian aliyepata medali hiyo baada kushinda mbio za mita 3000 ameeleza kufurahishwa na ushindi huo kwani alijiandaa na kuzingatia maelekezo ya walimu wake yaliyompelekea kupata ushindi huo na ameshauri vijana kama yeye kuthubutu na kuamini kuwa wanaweza kwani mchezo huo ni mzuri na una mafanikio makubwa.

medali
Medali ya shaba katika mashindano ya riadha iliyoletwa na kijana Francis imerejea tena baada ya miaka 19 tangu Tanzania iliposhinda medali hiyo mwaka 2008.

 

66 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/07/28/timu-ya-riadha-ya-umri-chini-ya-miaka-17-yarejee-nchini-na-ushindi/">
RSS