MWAKYEMBE AKABIDHI BENDERA KWA WACHEZAJI WA RIADHA

Julai 31

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe amekabidhi bendera kwa wachezaji 8 wa riadha wanaoenda kushindana katika mashindano ya London Marathon yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa 8  mjini London nchini  Uingereza, tukio hilo limefanyika  leo  Hyatt Regengy Kilimanjaro Hotel jijini Dar es salaam kwa maandalizi ya Maltichoice Tanzania  DSTV.

1501497574-PICHA 1
Mhe. Dr. Mwakyembe akizungumza na Wanariadha na Waandishi kabla ya kukabidhi bendera kuelekea katika mashindano ya London Marathon nchini Uingereza tukio lililiofanyika Haytt Regency Kilimanjaro Hotel jijini Dar es salaam mwazo wa wiki.

Waziri kabla ya kuwakabidhi bendera amewataka wanariadha hao kwenda kifuu mbele na kuleta ushindi kwani Watanzania wapo pamoja nao kuwaombea ili wapeperushe bendera vyema.

“Serikali inawakabidhi bendera kwa niaba ya Watanzania, tunawaombea mpeperushe bendera yetu vyema,’ alisema Waziri.

Aidha Dr. Mwakyembe amewataka Waandishi kuzitumia kalamu na kamera zao kama dhana ya maendeleo ya Michezo nchini.

 

44 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/07/31/mwakyembe-akabidhi-bendera-kwa-wachezaji-wa-riadha/">
RSS