WAKUZAJI NA WAANDAJI WA NGUMI ZA KULIPWA WATAKIWA KUFUATA TARATIBU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe amewataka wakuzaji  na waandaaji wa mapambano ya ngumi kufuata taratibu na sheria katika kuendesha mchezo huu nchini.

Rai hiyo ameitoa jana alipokutana na Kamati ya Utendaji ya chama cha ngumi za kulipwa Tanzania(TPBC) kilichosajiliwa kusimamia ngumi hizo nchini, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa uwanja wa Taifa Agosti 2 jioni jijini Dar es salaam.

Dr. Mwakyembe amesema kuwa katika kuendesha  Michezo kuna taratibu na sheria zilizowekwa na nchi lazima zifuatwe.

Aidha, amewataka TPBC  ndani ya miezi miwili mchakato wa kurekebisha katiba yao uwe umekamilika na kumwagiza Msajili aratibu mchakato wa kupitisha katiba hiyo na uchaguzi ufanyike.

Sambamba na hilo, Dr. Mwakyembe amesema kuwa wakuzaji na waandaaji wa mapambano yoyote wahakikishe kuwa wana kibali kutoka TPBC na BMT kabla ya kufanya hayo,au kutoka nje na kuingiza mabondia kutoka nje kinyume na hayo sheria itafuata mkondo wake.

“TPBC itakuwa mwavuli wa taasisi zote za ngumi za kulipwa nchini,” Alisisitiza Waziri Mwakyembe.

72 total views, 3 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/08/03/wakuzaji-na-waandaji-wa-ngumi-za-kulipwa-watakiwa-kufuata-taratibu/">
RSS