BMT YASAIDIA CHANETA KUPATA UONGOZI MPYA

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeratibu na kusimamia uchaguzi wa Chama cha Netiboli Tanzania uliofanyika Tarehe 30 Septemba, 2017 katika ukumbi wa NAM Hotel mjini dodoma.

22104488_1984049571808387_7622514992840562867_o
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Chaneta Dr. Devotha Marwa akila kiapo mbele ya Mwanasheria baada ya kutanganzwa ushindi.

Katika uchaguzi, Dk Devotha ndiye alipewa ridhaa na wapiga kura ya kuiongoza Chaneta kwa miaka minne akimshinda Damian Chonya.

kiapo ana
Makamu Mwenyekiti Mh. Anna Gidarya akila kiapo mbele ya mwanasheria baada ya kutangazwa ushindi.

Anna Giderya aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti akichukua nafasi ya Zainabu Mbiro ambaye kwenye uchaguzi wa sasa aliwania nafasi ya katibu mkuu lakini akaangushwa na Judith Ilunda huku Hilda Mwakatobe akiteuliwa kuwa Katibu msaidizi.

uongozi mpya wamekaa

Upande wa wajumbe, Mohamed Kilongozi, Luiza Jela, Yasinta Silvester, Fortunata Kabeja, Julieth Mndeme na Asha Sapi waliibuka kidedea na Grace Khatibu aliyekuwa anagombea nafasi ya mweka hazina akikosa baada ya kupigiwa kura nyingi za hapana.

22051146_1984061208473890_1425955925384467585_o
Waratibu wa uchaguzi kutoka Baraza wakiratibu zoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi wa Chama cha Netiboli jijini Dodoma

“Chaneta watafanya uchaguzi mdogo kuziba nafasi hiyo baadae,” alisema Kiganja akifafanua nafasi ya mweka hazina itakavyozibwa

pcha pamoja

Mkutano ulihudhuriwa na wajumbe 57, kutoka kwenye mikoa 21 nchini.  Aidha,uongozi utadumu madarakani kwa kipindi cha miaka minne (4) kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Netiboli Tanzania.

Baraza linawatakia uongozi mwema wenye kuleta mafanikio zaidi.

30 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/10/02/bmt-yasaidia-chaneta-kupata-uongozi-mpya/">
RSS