SERIKALI YAPOKEA UGENI WA WENYEJI WAO WA OLYMPIKI 2020

Wizara yenye dhamana ya Michezo pamoja Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wamepokea ugeni kutoka Mji wa Nagai nchini Japan ambao ni wenyeji wa Tanzania katika mashindano ya  Olympiki 2020.

IMG_0040

Ugeni huo umeongozwa na Meya wa Mji wa Nagai Bw. Shigeharu Uchiya na kupokelewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Omary Singo akiambatana na Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza  B. Benson Chacha na Viongozi wengine.

Meya wa Nagai Bw. Uchiya ameeleza kuwa, nia ya ujumbe huo ni kubadilishana uzoefu katika baadhi ya Michezo na Wakufunzi wa hapa nchini.

Hata hivyo, Meya huyo amesama kuwa, nchi ya Japan iko tayari kuisaidia Tanzania maandalizi ya Olyimpiki katika baadhi ya Michezo ikiwemo Judo, Baseball, Ngumi, Kuogelea, Riadha na Mpira wa Meza (Table Tenis) kwa kuleta Wakufunzi au kuziweka timu hizo nchini Japan kwa mazoezi zaidi ikikaribia Michuano hiyo.

IMG_0036

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo ameeleza kufurahisha sana na ujio na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Japan katika sekta mbalimbali ikiwemo Michezo.

Singo ameutaka ujumbe huo kuandaa andiko kuelezea nia yao na kuahidi kulifanyia kazi mapema.

Ujumbe huo baada ya kukutana na Uongozi wa Wizara na Baraza  unatarijia kukutana na Kamati ya Olyimpiki Tanzania (TOC) pamoja na baadhi Viongozi wa Vyama vya Michezo ikiwemo, Riadha, Judo, Ngumi, Kuogelea, na Baseball.

 

43 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/10/05/serikali-yapokea-ugeni-wa-wenyeji-wao-wa-olympiki-2020/">
RSS