WAZAZI ENDELEZENI NDOTO ZA WATOTO WENU 

Octoba, 19
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja (wa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa mchezo wa mpira wa basketi kutoka nchini Marekani baada ya kufungua mafunzo yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia Oct.19 hadi 21 katika kituo cha Michezo cha Symbion (JK park) jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja amewataka wazazi kuendeleza ndoto za watoto wao ili wafikie malengo yao.

Wito huo ameutoa leo wakati akifungua kliniki ya mchezo wa mpira wa  Basketi iliyoandaliwa na Serikali chini ya BMT kwa kushirikiana na chama cha mchezo huo Tanzania (TBA), kliniki itakayofanywa na Kocha wa Taifa Mchezo huo nchini Mmarekani Bw. Mathew Milollister Pamoja na wataalamu wenzake kutoka nchini hiyo.

Kliniki itakayofanyika kwa siku tatu (3) kuanzia leo  katika kituo cha michezo cha Rais Mstaafu Jakaya Kikwete cha “Symbion JK park” ikihusisha Vijana kutoka sehemu tofautia za Tanzania watakaoandaliwa ambapo watateuliwa wenye uwezo na kupata ufadhili wa kupatiwa mafunzo zaidi nchini Marekani.

Aidha, Katibu wa Baraza Bw. Kiganja amewaeleza wachezaji hao kuwa, hawana budi kuwatumia wataalamu hao ipasavyo kwani Taifa linategemea kupata timu bora baada ya mafunzo hayo na baadae nchini Marekani kwa watakaofanikiwa kuchaguliwa kwa ufadhili wa nchini huko.

IMG-20171020-WA0002

Kiganja amewaeleza vijana hao kuwa kazi ya Serikali ni kuwaletea wataalamu na kuwataka kuonesha nidhamu na kutoogopa kuuliza maswali ili kupata uelewa zaidi.

“Kazi yetu ni kuleta wataalamu, onesheni nidhamu, ulizeni maswali mpate kuelewa na msicheze kwa kumkomoa mtu”, alisema Kiganja na kuongeza kuwa;

“Usiogope kuuliza, kuuliza ndiyo kujua ili uchaguliwe kusoma Marekani na lengo lenu liwe lazima nichaguliwe,”Alisisitiza.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja (wa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa mchezo wa mpira wa basketi kutoka nchini Marekani baada ya kufungua mafunzo yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia Oct.19 hadi 21 katika kituo cha Michezo cha Symbion (JK park) jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja (wa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa mchezo wa mpira wa basketi kutoka nchini Marekani baada ya kufungua mafunzo yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia Oct.19 hadi 21 katika kituo cha Michezo cha Symbion (JK park) jijini Dar es salaam.

Katika hatua nyingine Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Michael Marwa amewataka wachezaji hao kuonesha ushirikiano kwa wataalamu hao ili mchezo uzidi kuwa na kiwango bora na kuleta sifa kwa Taifa katika mashindano mbalimbali.

48 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/10/19/wazazi-endelezeni-ndoto-za-watoto-wenu/">
RSS