CHAMA CHA MASHUA KUPATA ENEO LA KUJENGA KITUO CHA MAFUNZO

Na Frank M Mgunga

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta HARRISON MWAKYEMBE amesema atakisaidia chama cha mashua nchini(TSAA) kupata sehemu ya kujenga kituo cha mafunzo kwa mchezo wa mashua ili kukuza mchezo huo unaokua kwa kasi hapa nchini.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta HARRISON MWAKYEMBE akizungumza na viongozi wa Chama cha Mashua(TSAA)
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta HARRISON MWAKYEMBE akizungumza na viongozi wa Chama cha Mashua(TSAA)

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa chama cha Mashua nchini  na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,kilichofanyika tarehe 23/10/2017 katika ukumbi wa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

“kwa ajili ya kuendelea kukuza mchezo wa Mashua nchini ambao naamini utaletea sifa kubwa Taifa la Tanzania siku za usoni, nitawasaidia kupata eneo la kujenga kituo cha mafunzo cha mchezo wa Mashua,ili Taifa lielimike katika mchezo huo.”Alisema Mh. Mwakyembe.

Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akisoma kipeperushi cha Chama cha Mashua(TSAA)
Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akisoma kipeperushi cha Chama cha Mashua(TSAA)

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mashua FILIMON NASSARI amemshukuru Mh. Mwakyembe kwa kuwaahidi kuwasaidia kupata eneo la kujenga kituo cha mafunzo kwani wamekuwa na changamoto ya muda mrefu kupata eneo hilo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mashua(TSAA) Filimon Nassari akimshukuru Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe
Mwenyekiti wa Chama cha Mashua(TSAA) Filimon Nassari akimshukuru Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe

“Nakushukuru sana Mheshimiwa waziri, kwa kutuahidi ushirikiano wa kutusaidia kupata eneo la kujenga kituo cha mafunzo kwa mchezo wa mashua, kwani ni chachu ya kuendelea kukuza mchezo huu hapa nchini na kuliletea sifa Taifa la Tanzania siku za usoni,”Alisema Nassari.

36 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/10/24/chama-cha-mashua-kupata-eneo-la-kujenga-kituo-cha-mafunzo/">
RSS