UONGOZI WA ZAMANI WA CHANETA WAKABIDHI OFISI

Uongozi wa Zamani wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) chini ya mwenyekiti wake mstaafu Mama ANNA FAITH KIBIRA umekabidhi ofisi kwa viongozi wapya wa chama hicho tarehe 23/10/2017,makabidhiano yaliyofanyika katika ukumbi wa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

DSC_0059

Akikabidhi baadhi ya vifaa vya ofisi ya Chaneta kwa uongozi mpya, Mama Kibira amelishukuru Baraza la Michezo Taifa (BMT) kwa ushirikiano lililoonesha katika utendaji kazi wa Chama hicho kwa kipindi chote uongozi wake ulipokuwa madarakani ukiwemo na uchaguzi ambao umepelekea kupatikana viongozi wapya.

Baadhi ya Vifaa vilivyokabidhiwa kwa uongozi mpya CHANETA.
Baadhi ya Vifaa vilivyokabidhiwa kwa uongozi mpya CHANETA.

“Napenda kulishukuru sana Baraza la Michezo Taifa(BMT) chini ya katibu Mtendaji MOHAMMED KIGANJA kwa ushirikiano mkubwa lililotuonyesha kwa kipindi chote tulichokuwa madarakani mpaka sasa tumefanya uchaguzi na kumpata kiongozi mpya ambae ataendelea kuendeleza mchezo wa netiboli Tanzania,”Alisema Kibira.

Kwa upande wake mwenyekiti mpya wa CHANETA Dokta DEVOTHA JOHN MARWA ameushukuru uongozi uliopita kwa kazi nzuri na hatua ambayo wamepiga katika kuendeleza mchezo wa netiboli nchini Tanzania.

Mwenyekiti mpya wa CHANETA Dkt.Devotha Marwa akizungumza kuushukuru uongozi uliopita kwa kazi nzuri na hatua waliyopiga kuundeleza mchezo wa netiboli nchini na kuahidi kuendeleza mchezo huo kwa faida ya Taifa.
Mwenyekiti mpya wa CHANETA Dkt.Devotha Marwa akizungumza kuushukuru uongozi uliopita kwa kazi nzuri na hatua waliyopiga kuundeleza mchezo wa netiboli nchini na kuahidi kuendeleza mchezo huo kwa faida ya Taifa.

“Naushukuru sana uongozi uliopita kwa kazi na hatua ambayo wamepiga katika kukiongoza chama cha Netiboli Tanzania pamoja na kuhakikisha kuwa mchezo wa netiboli unakuwa katika Nyanja mbalimbali kuanzia mashuleni mpaka katika sekta nyingine hapa nchini,Nasi kama uongozi mpya tutahakikisha tunaendeleza kazi mliyokuwa mnaifanya na kupiga hatua zaidi,”Alisema Devotha.

 

115 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/10/24/uongozi-wa-zamani-wa-chaneta-wakabidhi-ofisi/">
RSS