YANGA KUANDIKA BARUA KWA WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (RITA)

Klabu ya yanga imetakiwa kuandika barua kwa wakala wa usajili,ufilisi na udhamini (RITA), kuhusu klabu hiyo kukosa Bodi ya wadhamini na ina mkakati gani kuhusu suala hilo kwani ni kinyume cha sheria na katiba.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta HARRISON MWAKYEMBE akizungumza na viongozi na wadau wa Klabu ya Yanga
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akizungumza na viongozi na wadau wa Klabu ya Yanga

Hayo yamesemwa na waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta HARRISON MWAKYEMBE katika mkutano uliowakutanika viongozi pamoja na wadau wa klabu ya Yanga katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

“Nataka nyinyi kama viongozi wa klabu ya Yanga muandike barua kwenda kwa wakala wa usajili,ufilisi na udhamini(RITA) kuwa klabu yenu haina Bodi ya wadhamini na hatua gani ambazo mtachukua kuitatua changamoto hiyo kabla ya mwezi wa kumi na mbili mwaka 2017,” Alisema Dokta Mwakyembe.

wakala wa usajili,ufilisi na udhamini(RITA) akifafanua jambo
wakala wa usajili,ufilisi na udhamini(RITA) akifafanua jambo

Kwa upande wake mwenyekiti wa muda wa klabu ya Yanga Clement Sanga, amekiri kuwepo changamoto hiyo ya klabu kukosa wadhamini na kumuahidi Mh. Mwakyembe kulifanyia kazi suala hilo kama katiba inavyoitaji kabla ya mwezi disemba mwaka 2017.

Mwenyekiti wa muda wa klabu ya yanga Clement Sanga akimshukuru Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe
Mwenyekiti wa muda wa klabu ya yanga Clement Sanga akitolea ufafanuzi suala la klabu ya yanga kukosa wadhamini

“Ni kweli mheshimiwa waziri tuna changamoto kubwa ya klabu kukosa wadhamini,tutawaandikia RITA barua,ila pia tunahaidi kama klabu kulifanyia kazi suala hilo na kulipatia ufumbuzi kabla ya muda tuliopewa kumalizika,”Alisema Sanga.

37 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/10/24/yanga-kuandika-barua-kwa-wakala-wa-usajili-ufilisi-na-udhamini-rita/">
RSS