MHESHIMIWA HARRISON MWAKYEMBE KUONGOZA KAMATI YA MAANDALIZI (AFCON U17) 2019.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe ametangaza kamati ya maandalizi ya michuano ya kombe la Mataifa Barani Africa kwa vijana wenye umri chini ya miaka kumi na saba(AFCON U17) itakayofanyika nchini Tanzania mwaka 2019.

Mheshimiwa Harrison Mwakyembe(katikati) akisoma majina yaliyoteuliwa ya kamati ya maandalizi ya michuano ya AFCON U17 2019, kushoto kwake ni Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na kulia ni Mjumbe wa CAF Leodgar Tenga.
Mheshimiwa Harrison Mwakyembe(katikati) akisoma majina yaliyoteuliwa ya kamati ya maandalizi ya michuano ya AFCON U17 2019, kushoto kwake ni Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia na kulia ni Mjumbe wa CAF Leodgar Tenga.

Mheshimiwa Mwakyembe ametangaza kamati hiyo leo tarehe 11/11/2017 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, ambapo kamati hiyo itaongozwa na Mheshimiwa Mwakyembe kama mwenyekiti,Leodgar Tenga (Makamu mwenyekiti),Henry Tadau (Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na wajumbe wengine ni:

1. Mheshimiwa Paul Makonda(Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam)
2. Mheshimiwa Hamisi Kigwangala(Waziri wa Maliasili na Utalii)
3. Michael Wambura(Makamu wa Rais TFF)
4. Dokta Damas Ndumbaro(Mkuu wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu Uria)
5. Dokta Francis Michael (Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Kitengo Cha Sheria)
6. Mohamed Dewji(Mkurugenzi na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group)
7. Abubakar Bakhresa(Mkurugenzi mtendaji wa Said Salim Bakhresa Company Limited)
8. Dokta Yusufu Singo Omary(Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Tanzania)
9. Alhaj Ahmed Mgoyi (Mwenyekiti wa kamati ya mashindano TFF)
10. Khalid Abdallah (Mwenyekiti kamati ya maendeleo ya vijana TFF),
11. Nasibu Mbaga (Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke)
12. Angetile Osiah( Mwananchi Communication),
13. Dokta Allan Kijazi(Mkurugenzi Mkuu TANAPA),
14. Doto James(Katibu mkuu Wizara ya Fedha),
15. Dokta Makakala (Kamishna Generali idara ya Uhamiaji),
16. Freddy Safieli Manongi (Mkurugenzi mtendaji Ngorongoro),
17. Lameck Nyambaya (Mjumbe TFF),
18. William Erio (Mkurugenzi wa PPF),
19. Kelvin Twisa (Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania)
20. Profesa Lawrence Museru (Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
21. Ladislaus Matindi ( Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL)
22. Dokta Devotha Mdachi (Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB).

23376111_2002145666665444_6471221284917582295_n

Aidha mheshimiwa Mwakyembe amesema kamati hiyo itaanza majukumu yake mara moja ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na michuano mizuri ya (AFCON U17) 2019 kama wenyeji wa michuano hiyo.

“kiukweli kamati hii tumeichagua iweze kuanza kazi ya maandalizi ya michuano ya AFCON U17 2019 mara moja kama waandaaji, ili tuweze kuwa na michuano mizuri na kuhakikisha tunafanya vizuri kitimu kama nchi katika michuano hiyo,”Alisema Mwakyembe.

54 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/11/11/mheshimiwa-harrison-mwakyembe-kuongoza-kamati-ya-maandalizi-afcon-u17-2019/">
RSS