UWANJA WA TAIFA KUANZA KUTUMIKA TENA 21/11/2017 BAADA YA MATENGENEZO SEHEMU YA KUCHEZEA MPIRA “PITCH”

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe ameridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa eneo la kuchezea mpira “Pitch” la Uwanja wa Taifa wakati wa ziara yake tarehe 11/11/2017 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na msimamizi mkuu wa marekebisho ya uwanja Alessio Giovanni Roso wakati wa ziara ya ukaguzi wa uwanja wa Taifa.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na msimamizi mkuu wa marekebisho ya uwanja Alessio Giovanni Roso wakati wa ziara ya ukaguzi wa uwanja wa Taifa.

Akizungumza katika ziara hiyo ya kukagua hatua iliyofikiwa katika matengenezo ya uwanja huo, Waziri Mhe.Dkt. Mwakyembe amesema kuwa amefurahishwa na hatua iliyofikiwa ya ukarabati ambapo sasa uwanja huo utakuwa tayari kwa matumizi tarehe 21/11/2017.

“Nimefurahishwa na mabadiliko niliyoyaona katika hatua hii,naamini ukarabati huu utafungua milango kwa mechi za kimataifa ikiwemo mashindano ya AFCON U17 yanayoratajiwa kufanyika nchini mwaka 2019,” alisema Dkt.Mwakyembe.

Msimamizi mkuu wa marekebisho ya uwanja Alessio Giovanni Roso akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya Michezo Yusuf Singo wakati wa ziara ya ukaguzi wa uwanja wa Taifa.
Msimamizi mkuu wa marekebisho ya uwanja Alessio Giovanni Roso akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya Michezo Yusuf Singo wakati wa ziara ya ukaguzi wa uwanja wa Taifa.

Aidha Dkt. Mwakyembe ameushukuru uongozi wa SPORTPESA kwa kuonyesha ushirikiano wa karibu na Serikali katika kuhakikisha inaweka mchango wake katika michezo kwa kukarabati sehemu ya kuchezea mpira “pitch” ya Uwanja wa Taifa pamoja na vifaa mbalimbali vilivyotolewa katika kuhakikisha kazi hiyo inakamilika.

Kwa upande wake msimamizi mkuu wa ukarabati wa uwanja Alessio Giovanni Roso amesema uwanja huo utakuwa tayari kuanza kutumika baada ya siku kumi kuanzia tarehe 11/11/2017 kwani nyasi tayari zimeota vizuri na pia wapo vijana wa kitanzania ambao wamewapa mafunzo maalumu juu ya usimamizi wa uwanja huo, ili uwe katika hali nzuri siku zote.

50 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/11/11/uwanja-wa-taifa-kuanza-kutumika-tena-21112017-baada-ya-matengenezo-sehemu-ya-kuchezea-mpira-pitch/">
RSS