KIGANJA: TUNAJIVUNIA KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA YA WANAWAKE KUELEKEA OLIMPIKI 2020 TOKYO JAPAN

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohamed Kiganja amesema Tanzania kupitia Baraza la Michezo kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Mashirikiano la kimataifa la Japan(JICA) nchini, inajivunia kuandaa mashindano ya Riadha ya wanawake kuelekea Olimpiki 2020 Tokyo Japan, ambayo yanashirikisha wanariadha kutoka mikoa 31 nchini yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 25-26 Novemba 2017 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohamed Kiganja akielezea ni jinsi gani Tanzania kupitia Baraza la Michezo kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Mashirikiano la kimataifa la Japan(JICA) nchini, inajivunia kuandaa mashindano ya Riadha ya wanawake kuelekea Olimpiki 2020 Tokyo Japan

Katibu Kiganja amesema Tanzania haijawahi kuandaa mashindano ya Riadha ya wanawake, hivyo ni jambo kubwa sana nchini na mpaka sasa yamefanikiwa kwa asilimia 92% baada ya mikoa 27 kati ya 31 kuthibitisha kushiriki katika mashindano hayo huku mikoa minne ikiwa bado haijatuma majina ya washiriki wake ambayo ni Lindi,Rukwa,Katavi pamoja na Iringa.

“Kiukweli ni jambo kubwa sana kwa nchi yetu ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la JICA kutoka nchini Japan kuandaa mashindano kama haya, na mpaka sasa naweza kusema yamefanikiwa kwa asilimia 92% baada ya mikoa 27 kati ya 31 kuthibitisha kushiriki katika mashindano huku mikoa minne ikiwa bado haijatuma majina ya washiriki wake ikiwa ni Lindi,Rukwa,Katavi pamoja na Iringa,”Alisema Kiganja.

Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha RiadhaTanzania (RT) Ombeni Zavala akielezea jinsi uongozi wa Riadha ulivyofurahi na kushukuru sana Serikali ya Tanzania na JICA kwa kubuni na kuendesha mashindano ya Riadha ya wanawake nchini kwani vipaji vingi vitaibuliwa na Tanzania itaweza kung’ara katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha.

Kwa upande wake mwakilishi Mkuu na Mkurugenzi wa Shirika la JICA nchini, Toshio Nagase amesema Tanzania katika mchezo wa Riadha na Mitupo kwa upande wa wanawake haijafanya vizuri kwa muda mrefu tangu iliposhinda medali ya kwanza mwaka 1965 Nchini Congo Brazzaville kupitia Theresa Dismas ambaye ndio alikuwa mwanamke wa kwanza kuchukua medali wakati wanaume wakiwa hawajapata chochote, hivyo basi tukio hili lenye kauli mbiu WANAWAKE KWANZA ni la kwanza kurudisha kumbukumbu zilizosahaulika miaka ya 60 na kudhihirisha duniani kuwa wanariadha wanawake wanaweza kufanya makubwa katika mchezo wa Riadha endapo kama watapewa motisha na mafunzo mazuri.

“Tanzania katika Mchezo wa Riadha na Mitupo kwa upande wa wanawake, haijafanya vizuri kwa muda mrefu sana tangu iliposhinda medali ya kwanza mwaka 1965 nchini Congo Brazzaville kupitia Theresa Dismas hivyo basi tukio hili ni la kwanza kurudisha kumbukumbu zilizosahaulika miaka ya 60 na kudhihirisha duniani wanariadha wanawake wanaweza kufanya makubwa katika mchezo wa Riadha kama watapewa motisha na mafunzo mazuri,”Alisema Nagase.

Mkurugenzi wa Shirika la JICA nchini, Toshio Nagase akielezea ni jinsi gani Tanzania katika mchezo wa Riadha na Mitupo kwa upande wa wanawake haijafanya vizuri kwa muda mrefu tangu iliposhinda medali ya kwanza mwaka 1965 Nchini Congo Brazzaville kupitia Theresa Dismas

Nae Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha RiadhaTanzania (RT) Ombeni Zavala amesema uongozi wa Riadha umefurahi na kushukuru sana Serikali ya Tanzania na JICA kwa kubuni na kuendesha mashindano ya Riadha ya wanawake nchini kwani vipaji vingi vitaibuliwa na Tanzania itaweza kung’ara katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha.

“Uongozi wa Riadha umefurahi na kushukuru sana Serikali ya Tanzania na JICA kwa kubuni na kusaidia kuendesha mashindano ya Riadha ya wanawake nchini kwani vipaji vingi vitaibuliwa na Tanzania itaweza kung’ara katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha,”Alisema Ombeni

513 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/11/21/kiganja-tunajivunia-kuandaa-mashindano-ya-riadha-ya-wanawake-kuelekea-olimpiki-2020-tokyo-japan/">
RSS