IBRAHIM CLASS “KING MAWE” ATETEA TAJI LAKE LA GBC KWA KUMDUNDA KOOS SIBIYA KUTOKA AFRIKA KUSINI.

Na Frank M Mgunga
Bondia Mtanzania, Ibrahim Class Mgendera almaarufu kama King mawe amefanikiwa kutetea taji lake GBC uzito wa Light baada ya kumshinda kwa pointi Bondia Koos Sibiya kutoka nchini Afrika Kusini.

Mgendera ameshinda kwa pointi za majaji wote, ingawa ushindi wake umelalamikiwa na mpinzani wake baada ya pambano hilo.

Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpongeza Bondia Ibrahim Class baada ya kuibuka mshindi katika pambano la ngumi la kimataifa lenye mizunguko kumi na mbili dhidi ya Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini, Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpongeza Bondia Ibrahim Class baada ya kuibuka mshindi katika pambano la ngumi la kimataifa lenye mizunguko kumi na mbili dhidi ya Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini, Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo.

Bondia huyo aliye chini ya Joe Gym Kawe jijini Dar es salaam hakuwa na kazi nyepesi ulingoni, kwani alikutana na bondia mzoefu na mwenye ngumi nzito – lakini akahimili vishindo vyote na kuwafurahisha Watanzania wachache waliojitokeza Uwanja wa Uhuru kumshangilia kwa mchezo mzuri huku akipiga ngumi za kudonoa kwa wingi katika staili yake ya Orthodox.

Dalili za Ibrahimu Class kushinda pambano hilo zilianza kuonekana raundi ya nane baada ya kumjeruhi kwenye pua Sibiya ambaye alivuja damu eneo hilo hadi mdomoni.

Image may contain: 3 people, people smiling, people sitting
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo (katikati) na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja wakifurahia pambano la ngumi kati ya mtanzania Ibrahim Class dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika Kusini

Class aliyezaliwa Oktoba 10, mwaka 1990 eneo la Ipogolo, wilayani Mufindi Mkoani Iringa, alitwaa taji hilo Julai 1, mwaka huu baada ya kumpiga Jose Luis Forero Atencio wa Panama kwa pointi Jijini Berlin, Ujerumani.

Hili linakuwa pambano la 21 kwa bondia huyo kuweza kushinda kati ya 25 aliyocheza huku akiwa amepoteza mapambano manne ulingoni.

22 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/11/25/ibrahim-class-king-mawe-atetea-taji-lake-la-gbc-kwa-kumdunda-koos-sibiya-kutoka-afrika-kusini/">
RSS