MWAKYEMBE: WANARIADHA SHINDANENI KWA MALENGO NA MASLAHI YA TAIFA.

Na Frank M Mgunga
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe amefungua mashindano ya Taifa ya Riadha kwa Wanawake yanayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa kushirikisha wanariadha kutoka Mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akifyatua risasi hewani kuonyesha ishara ya ufunguzi wa mashindano ya Taifa ya Riadha kwa Wanawake yanayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Mwakyembe amefungua mashindano hayo na kuwataka wanariadha washiriki kushindana kwa malengo na maslahi ya kuisaidia Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa siku za usoni.

Wanariadha wanawake kutoka kanda ya kaskazini wakichuana vikali katika mbio za mita elfu kumi
Wanariadha wanawake kutoka kanda ya kaskazini wakichuana vikali katika mbio za mita elfu kumi

Hata hivyo Mheshimiwa Mwakyembe amelishukuru Shirika la Mashirikiano ya kimataifa la Japan (JICA) ambalo limewezesha kufanyika kwa mashindano hayo, kwa lengo la kuiwezesha Tanzania kuwa na washiriki wengi wanawake kwenye Mashindano ya Olimpiki 2020 yatakayofanyika mjini Tokyo nchini Japan.

“Nalishukuru sana Shirika la Mashirikiano ya kimataifa la Japan (JICA) ambalo limewezesha kufanyika kwa mashindano haya, lengo likiwa ni kuiwezesha Tanzania kuwa na washiriki wengi wanawake kwenye Olimpiki ya 2020 itakayofanyika Tokyo nchini Japan,”Alisema Mwakyembe

210 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/11/25/mwakyembe-wanariadha-shindaneni-kwa-malengo-na-maslahi-ya-taifa/">
RSS