ARUSHA VINARA MASHINDANO YA RIADHA YA WANAWAKE KUELEKEA OLIMPIKI 2020 TOKYO NCHINI JAPAN.

Na Frank M Mgunga
Mashindano ya Riadha ya wanawake kuelekea Olimpiki 2020 Tokyo nchini Japan yamefikia tamati leo tarehe 26 Novemba 2017 katika uwanja wa Taifa jijini Dar e s salaam kwa Mkoa wa Arusha kuibuka kidedea baada ya kujinyakulia jumla ya medali 6 zikiwemo za Dhahabu 2 Fedha 3 na Shaba 1.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja akiwavisha medali washindi wa Mita mia Moja ambao ni WINFRIDA MAKENJI kutoka Dar es salaam (Dhahabu), KAZIJA H. SIMAI kutoka Mjini Magharibi na NASRA ABDALLAH kutoka Kaskazini Pemba.

Akifunga mashindano hayo ya siku mbili mgeni rasmi Bw.Hiroshi Kato ambaye ni makamu wa kwanza wa Rais wa Shirika la Mashirikiano la Kimataifa la Japan (JICA) amesema amefurahi sana kuja Tanzania kuangalia Mashindano hayo yaliyobeba kauli mbiu “LADIES FIRST” yani Wanawake Kwanza sambamba na kuzishukuru kampuni za kijapani kwa kufadhili sehemu ya mashindano hayo kama vile malazi na chakula huku akisema kuwa mafanikio ya mashindano hayo ni matokeo ya ushirikiano mkubwa sana kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Baraza la Michezo la Taifa,Mikoa na JICA.

“Nimefurahi sana kuja Tanzania kuangalia mashindano haya ya LADIES FIRST, lakini pia nazishukuru kampuni za kijapani kwa kufadhili sehemu ya mashindano haya kama vile malazi na chakula bila kusahau kuwa mafanikio ya mashindano ni matokeo ya ushirikiano kati ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Baraza la Michezo la Taifa, Mikoa na JICA,”Alisema Kato.

Bw.Hiroshi Kato makamu wa kwanza wa Rais wa Shirika la Mashirikiano la Kimataifa la Japan (JICA) akikabidhi zawadi ya kikombe kwa mwakilishi wa washindi wa pili Mkoa wa Dar es salaam.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja ameushukuru uongozi wa JICA kwa kuandaa mashindano ya Riadha ya Wanawake Jambo ambalo limeibua vipaji kwa Wanawake ambao sasa wataendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali ya kimataifa na hatimaye kupata washindi ambao wataiwakilisha nchi katika michuano ya Olimpiki 2020 Tokyo nchini Japan.

Rais wa Shirika la Mashirikiano la Kimataifa la Japan (JICA) Bw.Hiroshi Kato akimkabidhi Zawadi ya Kombe mwakilishi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kama washindi wa Tatu.

“Naushukuru sana uongozi wa JICA kwa kuandaa mashindano haya kwani imekuwa ni chachu kubwa ya kuibua vipaji ambavyo tumeviona na huu ni mwanzo mzuri kwa nchi yetu ya Tanzania kuandaa kufanya mashindano kama haya na tunaamini kuwa sasa tutaanza kupata medali katika mashindano mbalimbali ya Riadha,lakini pia tutahakikisha washiriki hawa wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya kimataifa na hatimaye kupata washindi ambao wataiwakilisha nchi katika michuano ya Olimpiki 2020 Tokyo nchini Japan,”Alisema Kiganja.

95 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/11/26/arusha-vinara-mashindano-ya-riadha-ya-wanawake-kuelekea-olimpiki-2020-tokyo-nchini-japan/">
RSS