WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA VIFAA VYA MICHEZO KWA AJILI YA KUANZISHA LIGI MAALUM KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM.

Na Frank M Mgunga

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amepokea vifaa vya Michezo vikiwemo mipira, jezi na viatu vyenye thamani ya shilingi Milioni Hamsini fedha taslimu kutoka kwa mfanyabiashara Maarufu Visiwani Zanzibar Mohammed Raza, katika hafla fupi iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kuanzisha Ligi maalum ya Mpira wa Miguu kwa majimbo kumi ya Mkoa wa Dar es salaam.

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda Zawadi ya Kikombe kwa atakayekuwa Mshindi wa kwanza katika mashindano ya Mpira wa miguu Ligi Maalum itakayoanzishwa Jijini Dar es salaam, Pembeni mwenye Suti ya Kijani ni Mfanyabiashara Maarufu wa Zanzibar Mohammed Raza aliyetoa Vifaa Hivyo.

Baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Mheshimiwa Majaliwa alivikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye ndiye atakuwa akisimamia Ligi hiyo ambayo ameagiza ianze mara moja kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya wachezaji mbalimbali wanaochipukia hapa nchini pamoja na kuwaepusha vijana kukaa vijiweni sambamba na kuweka mpango endelevu wa Michezo katika eneo husika.

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akikagua vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mfanyabiashara maarufu kutoka Zanzibar Mohammed Raza

“Naagiza ligi hiyo ianzishwe mara moja kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya wachezaji mbalimbali wanaochipukia hapa nchini pamoja na kuwaepusha vijana kukaa vijiweni sambamba na kuweka mpango endelevu wa Michezo katika Eneo husika,”Alisema Majaliwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda amemshukuru Bw. Raza kwa kutoa vifaa hivyo kwani mashindano hayo yanaenda kuongeza hamasa kubwa na kupunguza matatizo ya magonjwa ambayo yangeweza kuepukika endapo vijana wangekuwa wanajishughulisha na mazoezi.

mkuu4

“Namshukuru sana Bw. Raza kwa kutoa vifaa hivi kwani mashindano ambayo tunaenda kuyaanzisha yataongeza hamasa kubwa na kupunguza matatizo ya magonjwa ambayo yangeweza kuepukika endapo vijana wangekuwa wanajishughulisha na mazoezi,”Alisema Makonda.

131 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/11/28/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-apokea-vifaa-vya-michezo-kwa-ajili-ya-kuanzisha-ligi-maalum-katika-mkoa-wa-dar-es-salaam/">
RSS