MAFANIKIO YA MIKAKATI MINNE YA CHAMA CHA MCHEZO WA BASEBALL TANZANIA (TaBSA)

Katibu Mkuu wa Chama Baseball na SoftBall Tanzania(TaBSA) Alphelio Nchimbi amesema kwa mwaka huu 2017 walikuwa na mikakati Mikuu Minne ambayo wamefanikiwa kutimiza kwa kipindi cha muda mfupi ambayo ni kushiriki ipasavyo mkutano mkuu wa shirikisho la mchezo wa Baseball na Softball la Dunia ambao ulifanyika Gaboroni Botswana ambapo walienda huko kupigania kupata uanachama wa kudumu wa shirikisho hilo ambapo walifanikiwa kati ya Tarehe 13 na 15 Oktoba 2017 na katika nchi saba zilizopata uanachama wa kudumu Tanzania ikiwa ni moja wapo.

Katibu Mkuu wa Chama Baseball na SoftBall Tanzania(TaBSA) Alphelio Nchimbi akielezea jinsi walivyofanikiwa kutimiza mikakati Mikuu Minne kwa kipindi cha muda mfupi mwaka huu 2017.

Aidha Bw. Nchimbi amesema wameweza kumkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe hati ya kuonyesha kuwa chama hicho kinatambulika kimataifa na wapo katika mikakati ya kutumia utambulisho huo kuhakikisha vijana wa Tanzania wanasonga mbele katika mchezo wa Baseball.

“Wiki iliyopita tumeweza kumkabidhi Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe hati ya kuonyesha kuwa chama chetu sasa kinatambulika kimataifa na tupo katika mikakati ya kutumia utambulisho huo kuhakikisha vijana wa Tanzania wanasonga mbele katika mchezo wa base ball,”Alisema Nchimbi.

Baadhi ya wachezaji wa Mchezo wa Baseball wakiwa katika Mazoezi ya mchezo huo unaoendelea kusambaa Nchini.

Kwa upande mwingine chama hicho katika mkakati wa pili kimefanikiwa kuendesha mafunzo ya mchezo wa Baseball na Softball ambayo yameendeshwa na wakufunzi wa shirikisho hilo jijini Mwanza kati ya Tarehe 22 hadi 26 Oktoba na yalifanikiwa kwa kuwa na washiriki wengi zaidi na wakufunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Michezo kama vile Mallya na Butimba, huku mkakati wa tatu ni kufanya mashindano ya Taifa ambayo yamefanyika kuanzia Tarehe 1 hadi 3 Disemba mwaka 2017, ambayo yameshirikisha timu 12 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania yaliohusisha vijana wenye umri chini ya miaka 18 kwa Timu ya Dodoma kuchukua ubingwa na mkakati wa Nne timu ya Taifa imeteuliwa katika mashindano hayo inaenda jijini Mwanza Tarehe 5 Disemba 2017 kushiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki.

64 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/12/04/mafanikio-ya-mikakati-minne-ya-chama-cha-mchezo-wa-baseball-tanzania-tabsa/">
RSS