BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA (BMT) LAUNGA MKONO JUHUDI ZA TPC KWA WATU WENYE ULEMAVU TANZANIA

Kamati ya Taifa ya Michezo ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu Tanzania(TPC) imeadhimisha siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu ambayo huadhimishwa kila ifikapo Tarehe 3 Disemba kila mwaka kwa kuandaa Tamasha la Michezo ya watu wenye ulemavu lililofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Mnazi mmoja na kujumuisha Michezo mbalimbali kama vile mpira wa kikapu na mpira wa pete.

Katibu wa TPC Tuma Dandi akizungumzia maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbiu “Mabadiliko tunapoelekea kwenye Jamii endelevu na Imara kwa Wote” yanafanyika katika mwamko wa kuridhiwa kwa malengo mapya ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa hadi ifikapo 2030
Katibu wa TPC Tuma Dandi akizungumzia maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbiu “Mabadiliko tunapoelekea kwenye Jamii endelevu na Imara kwa Wote” yanafanyika katika mwamko wa kuridhiwa kwa malengo mapya ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa hadi ifikapo 2030

Akizungumza katika ufunguzi wa Tamasha hilo mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Bi. Neema Msitha amesema Baraza la Michezo linaunga mkono juhudi zinazoonyeshwa na kamati ya Taifa ya Michezo ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu Tanzania kwani ibara ya 30 ya mkataba wa haki za watu wenye ulemavu inatoa fursa kwa watu wenye ulemavu kujihusisha na Michezo ambayo ni njia sahihi ya kujumuika na jamii, kulinda afya, kufurahi lakini pia kukuza vipaji na kujipatia fursa za ajira kupitia Michezo.
Aidha Bi. Neema amewaasa wanamichezo wenye ulemavu kuichukulia Michezo kama kitu binafsi chenye faida katika maisha yao ya kila siku kwani mafanikio yoyote watakayopata katika Michezo ni kwa ajili ya faida yao wenyewe na Taifa kwa ujumla.

Wachezaji wa Mchezo wa Mpira wa kikapu wakiwa katika Tamasha la Maadhimisho ya siku ya walemavu katika viwanja vya JK Mnazi mmoja.
Wachezaji wa Mchezo wa Mpira wa kikapu wakiwa katika mchezo wa Tamasha la Maadhimisho ya siku ya walemavu katika viwanja vya JK Mnazi mmoja.

“Naomba muichukulie Michezo kama kitu binafsi ambacho kina faida katika maisha yenu ya kila siku kwani mafanikio yoyote mtakayopata michezoni ni kwa ajili ya faida yenu wenyewe na Taifa kwa ujumla,”Alisema Neema.
Kwa upande wake katibu wa TPC, Ndugu Tuma Provian Dandi amesema maadhimisho ya mwaka huu yenye kauli mbiu “Mabadiliko tunapoelekea kwenye Jamii endelevu na Imara kwa Wote” yanafanyika katika mwamko wa kuridhiwa kwa malengo mapya ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa hadi ifikapo 2030,huku mwongozo huo wa kimataifa ukiwataka kutomuacha mtu yeyote nyuma ili kuijenga dunia endelevu kwa ajili ya wote sambamba na kujumuisha masuala mengi ya kuwajali watu wenye ulemavu kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kuzibadilisha ahadi hizo kuwa katika vitendo.
“Ndugu mgeni Rasmi maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika katika mwamko wa kuridhiwa kwa malengo mapya ya maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa hadi ifikapo 2030,na mwongozo huu wa kimataifa unataka kutomuacha mtu yeyote nyuma ili kuijenga dunia endelevu kwa ajili ya wote sambamba na kujumuisha masuala mengi ya kuwajali watu wenye ulemavu kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kuzibadilisha ahadi hizo kuwa katika vitendo,”Alisema Dandi.

62 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/12/05/baraza-la-michezo-la-taifa-bmt-launga-mkono-juhudi-za-tpc-kwa-watu-wenye-ulemavu-tanzania/">
RSS