WAZIRI MWAKYEMBE: IBRAHIM CLASS NI BONDIA MZALENDO, MAHIRI NA SHUPAVU

Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imemkabidhi Bondia Ibrahim Class “King Mawe” hundi ya shilingi milioni kumi na nane na laki mbili kama zawadi yake ya ushindi wa pambano la ngumi la GBC lililopigwa Tarehe 25 Novemba 2017 ambapo Class aliweza kumshinda kwa Pointi mpinzani wake Koos Sibiya kutoka nchini Afrika Kusini.

mwakyembe
Mheshimiwa Harrison Mwakyembe akielezea lengo la kumkabidhi Ibrahim Class hundi yake mbele ya waandishi wa habari kwa umahiri,uzalendo na ushujaa aliouonesha kwa watanzania katika pambano lake dhidi ya Koos Sibiya sambamba na kuweza kushinda mataji mbalimbali ya ngumi duniani kama vile mkanda wa dunia wa “Middle Super Weight”.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe amesema lengo la kumkabidhi bondia huyo hundi yake mbele ya waandishi wa habari ni umahiri,uzalendo na ushujaa aliouonesha kwa watanzania katika pambano lake dhidi ya Koos Sibiya sambamba na kuweza kushinda mataji mbalimbali ya ngumi duniani kama vile mkanda wa dunia wa “Middle Super Weight”.

Aidha Mheshimiwa Mwakyembe amewataka Watanzania wote kujitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni ya kitaifa ya Uzalendo inayotarajiwa kuzinduliwa Tarehe 08 Desemba 2017 mjini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.

Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Wizara yake imeamua kuanzisha Kampeni ya Uzalendo ili kuwakumbusha watanzania kupenda,kujali na kuthamini nchi yao kwa kuenzi na kuupenda Utamaduni wa Taifa hilo ambao ndio unaounganisha na kutambulisha watanzania.

“Uzalendo wetu umetikisika ni lazima sasa kuamka na kujua kuwa tuna jukumu la kuenzi Uzalendo tuliojengewa na Waasisi wa Taifa letu wa kupenda nchi yetu na kudumisha Utamaduni wetu,”Alisema Mhe. Mwakyembe.

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari Juliana Shonza akizungumzia kuhusu Kampeni ya Uzalendo kuwa ni muhimu sana kwa Taifa letu kwa kuwa inalenga kukumbusha jamii Utamaduni wetu ambao ndio unafanya jamii kuwa na Uzalendo katika nyanja zote za maendeleo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza amesema Kampeni hiyo ni muhimu sana kwa Taifa letu kwakua inalenga kukumbusha jamii Utamaduni wetu ambao ndio unafanya jamii kuwa na uzalendo katika nyanja zote za maendeleo.

“Ili kufikia adhma ya Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda bila kuwa na uzalendo wa kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikiana.” Alisema Mhe. Juliana.

Mhe. Juliana ameongeza kuwa Wasanii wanahabari na wanamichezo wanajukumu kubwa sana la kutangaza Kampeni hii lakini pia kuelimisha jamii maana ya Uzalendo pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kutenda mambo mazuri yanayoendana na Utamaduni wa Tanzania kwani wao ni kioo cha jamii.

47 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/12/05/waziri-mwakyembe-ibrahim-class-ni-bondia-mzalendo-mahiri-na-shupavu/">
RSS