SERIKALI HAIJAACHA MCHEZO WA WUSHU

Na Najaha Bakari

Mkurugenzi wa Miundombinu ya Michezo kwa niaba ya Naibu Waziri mwenye dhamana ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kwamba Serikali haijaacha mchezo wa Wushu inautambua na kuuthamini na ndio maana imeingia mkataba na Serikali ya China kuuendeleza mchezo huu nchini na unafundishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia taasisi ya Comfucius.

Mkurugenzi wa Miundombinu ya Michezo kwa niaba ya Naibu Waziri mwenye dhamana ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akielezea kuwa Serikali haijaacha mchezo wa Wushu inautambua na kuuthamini na ndio maana imeingia mkataba na Serikali ya China kuuendeleza mchezo huu nchini na unafundishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupitia taasisi ya Comfucius.

Hayo ameyasema Jumapili ya Disemba 11 mwaka 2017 katika maafali ya nne ya chuo cha Shaolin Kung Fu Wushu pamoja na matawi yake ikiwemo klabu ya Kongowe Wushu,  Disu Nyara, Chalinze na Kisabi Wushu na kupata vyeo tofauti ikiwemo mikanda na vyeti.

“Serikali haijaacha mchezo wa Wushu inautambua na kuuthamini na ndio maana tumeingia mkataba na Serikali ya China na mchezo huu unafundishwa katika Chuo cha Dodoma kupitia taasisi yake ya Comfucius”alisema Nkenyenge.

Nkenyenge aliendelea kuwa katika mkataba huo tunatarajia kuwa na wataalamu wa Wushu wengi nchini kutoka katika mataifa mengi ambapo Vijana wengi watafaidika kwa kupata mafunzo yakiwemo ya darasani na michezo.

Hata hivyo Wizara katika mpango wake imeomba Serikali za Mikoa kutenga shule mbili mbili za Sekondari na Msingi ili kila mwanafunzi apate elimu na ajihusishe na mchezo wowote kwani michezo ni Afya, Ajira na hujenga umoja na mahusiano mazuri.

“Wizara katika mpango wake imeomba Serikali za Mikoa kutenga Shule mbili mbili Sekondari na Msingi ili wanafunzi wafaidike kwani Sisi kama Serikali tunaamini Michezo ni Afya, ni Ajira hujenga umoja na mahusiano mazuri kwa jimii”alisisitiza Nkenyenge.

Aidha, Nkenyenge amewataka  wanamichezo wa Chuo hicho Pamoja na matawi yake na wanamichezo wengine kuimarisha nidhamu katika michezo yao ili michezo isionekane niya wahuni na kutothaminiwa.

Makamu wa Rais wa chama cha Wushu cha Taifa Bw. Kawina Hadji Konde akielezea ni kwa jinsi gani wanaendelea kupigania chama cha Wushu cha Dunia (IWF) kiingie kwenye Olimpiki na kusema anaamini Vijana wao wako vizuri na wataleta sifa kwa Taifa.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa chama cha Wushu cha Taifa Bw. Kawina Hadji Konde amesema wanaendelea kupigania chama cha mchezo huu cha dunia (IWF)  kiingie kwenye Olimpiki na kusema anaamini Vijana wao wako vizuri wataleta sifa kwa Taifa.

Konde kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shaolin Kung Fu Wushu amesema wanao wataalamu wenye viwango vya Kimataifa ila changamoto walio nayo ni vifaa na Miondombinu na kuiomba Serikali kuwasaidia pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ya michezo.

Mmoja wa wahitimu wa mchezo wa Wushu akikabidhiwa Cheti cha Kuitimu mafunzo ya Awali na Mkurugenzi wa Miundombinu ya Michezo kwa niaba ya Naibu Waziri mwenye dhamana ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge
Mmoja wa wahitimu wa mchezo wa Wushu akikabidhiwa Cheti cha Kuitimu mafunzo ya Awali na Mkurugenzi wa Miundombinu ya Michezo kwa niaba ya Naibu Waziri mwenye dhamana ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge

Katika maafali hayo, watahiniwa 70 walihitimu katika ngazi tofauti za mikanda ambapo watahiniwa 40 kutoka Shaolin Kung Fu Wushu ya Mlandizi, 10 walitoka klabu ya Disu Dragon,  8 kutoka Klabu ya Kongowe, 2 Klabu ya Chalinze na 10 kutoka Kisabi.

Wahitimu 4 walifaulu kwa kupata mkanda mweusi, 40 walipata vyeti, ambapo waliobaki walifaulu kwa kuvalishwa mikanda ya njano.

40 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/12/10/serikali-haijaacha-mchezo-wa-wushu/">
RSS