MHESHIMIWA MWAKYEMBE AFAFANUA KANUNI NA SHERIA ZA BMT KUHUSU UWEKEZAJI NA UMILIKI WA KLABU ZA MPIRA WA MIGUU NCHINI.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe amefafanua kanuni na Sheria za Baraza la Michezo la Taifa kuhusu uwekezaji na umiliki wa klabu za mpira wa miguu nchini baada ya maswali mengi kuibuka kuhusu klabu ya simba baada ya mwekezaji Mohammed Dewji kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 49.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akifafanua kanuni na Sheria za Baraza la Michezo la Taifa kuhusu uwekezaji na umiliki wa klabu za mpira wa miguu nchini, kulia ni Msajili wa Vyama vya Michezo Ibrahim Sapi Mkwawa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akifafanua kanuni na Sheria za Baraza la Michezo la Taifa kuhusu uwekezaji na umiliki wa klabu za mpira wa miguu nchini, kulia ni Msajili wa Vyama vya Michezo Ibrahim Sapi Mkwawa.

Mheshimiwa Mwakyembe amesema klabu yoyote ambayo imeanzishwa na wanachama asilimia hamsini na moja lazima ziwehisa za wanachama na Arobaini na Tisa ziwe za mwekezaji, hivyo basi wamefanya maamuzi kupitia marekebisho ya kanuni za sheria ya Baraza la Michezo la Taifa ya mwaka 2017 ambayo yanaendana kwa pamoja na kanuni ya BMT ya mwaka 1999 na kuongeza kanuni mpya ya 18A (1) ambayo inasema  vyama au vilabu vya Michezo vilivyoanzishwa na wanachama vikiamua kuuza hisa zake vinapaswa kutenga asilimia hamsini na moja kwa ajili ya wanachama wake na asilimia Arobaini na Tisa kwa wanaotaka kununua.

“klabu yoyote ambayo imeanzishwa na wanachama asilimia hamsini na moja lazima ziwe hisa za wanachama na Arobaini na Tisa ziwe za mwekezaji, tumefanya maamuzi ya kupitia marekebisho ya kanuni za sheria ya BMT 2017 ambayo yanaendana kwa pamoja na kanuni ya BMT ya mwaka 1999,”Alisema Waziri Mwakyembe.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akifafanua kanuni na Sheria za Baraza la Michezo la Taifa kuhusu uwekezaji na umiliki wa klabu za mpira wa miguu nchini, kulia ni Msajili wa Vyama vya Michezo Ibrahim Sapi Mkwawa na kushoto mwenye koti Jeusi ni Mtendaji Mkuu wa TFF Wilfred Kidao.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akifafanua kanuni na Sheria za Baraza la Michezo la Taifa kuhusu uwekezaji na umiliki wa klabu za mpira wa miguu nchini, kulia ni Msajili wa Vyama vya Michezo Ibrahim Sapi Mkwawa na kushoto mwenye koti Jeusi ni Mtendaji Mkuu wa TFF Wilfred Kidao.

Aidha Mheshimiwa Mwakyembe amesema klabu inapoamua kuuza hisa zake lazima iingie kwenye mfumo wa hisa na maombi ya uuzaji na ununuzi wa hisa yatalazimika kuidhinishwa na chombo husika kinachosimamia mitaji na dhamana hapa Tanzania kwa mujibu wa Sheria za nchi.

Kwa upande mwingine Waziri Mwakyembe ameipongeza klabu ya Simba kwa mabadiliko waliyoamua ya kuruhusu uwekezaji  na kumpongeza Mohammed Dewji kwa kujitokeza kuwekeza katika klabu ya Simba, ila amesisitiza kuwa uwekezaji huo uendane na matakwa ya sheria za nchi.

“Naipongeza sana klabu ya Simba kwa mabadiliko waliyoamua ya kuruhusu uwekezaji na kumpongeza Mohammed Dewji kwa kujitokeza kuwekeza katika klabu ya Simba, ila uwekezaji huo uendane na matakwa ya sheria za nchi,”Alisema Mheshimiwa Mwakyembe.

42 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/12/13/mheshimiwa-mwakyembe-afafanua-kanuni-na-sheria-za-bmt-kuhusu-uwekezaji-na-umiliki-wa-klabu-za-mpira-wa-miguu-nchini/">
RSS