MWALUSAMBA KULIONGOZA SHIMIWI KWA AWAMU NYINGINE TENA

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limesaidia kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) uliofanyika Tarehe 16 Disemba 2017 katika ukumbi wa Mount Uruguru Hotel mjini Morogoro.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja akiwa anaratibu uchaguzi wa SHIMIWI Morogoro
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja akiwa anaratibu uchaguzi wa SHIMIWI Morogoro

Katika uchaguzi huo, Ndugu Daniel Zachariah Mwalusamba ndiye alipewa ridhaa na wapiga kura ya kuliongoza SHIMIWI kama mwenyekiti kwa Awamu nyingine ya miaka mitatu baada ya kupata kura 42 kati ya kura 44 zilizopigwa.

Ndugu Daniel Zachariah Mwalusamba akila kiapo kuwa Mwenyekiti Mpya wa SHIMIWI mbele ya Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja (kulia) na Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzania ambaye pia ni Wakili (kushoto)
Ndugu Daniel Zachariah Mwalusamba akila kiapo kuwa Mwenyekiti Mpya wa SHIMIWI mbele ya Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja (kulia) na Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzania ambaye pia ni Wakili (kushoto)

Ally Lucas Katembo aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 41 kutoka kwa wajumbe baada ya kugombea nafasi hiyo pekeake hivyo kurejea tena kwa awamu nyingine baada ya kuongoza nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, huku kwa upande wa nafasi ya Katibu Mkuu Ndugu Moshi Makuka ameibuka kidedea baada ya kumshinda Andrew Sekimweri kwa kupata kura 38 dhidi ya kura 6 alizopata mpinzani wake.

Ndugu Ally Katembo akila kiapo kuwa Mwenyekiti Mpya wa SHIMIWI mbele ya Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja (kulia) na Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzania ambaye pia ni Wakili (kushoto)
Ndugu Ally Katembo akila kiapo kuwa  Makamu Mwenyekiti Mpya wa SHIMIWI mbele ya Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja (kulia) na Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzania ambaye pia ni Wakili (kushoto)

Upande wa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Ndugu Alex Faustine Temba alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 29 akimshinda Margreth Mtaki aliyepata kura 15, Nafasi ya Mhazini ilichukuliwa na William Mgaya Mkombozi aliyemshinda Frank Kibona kwa kura mbili za wajumbe baada ya kupata kura 23 kwa 21 hivyo Mkombozi kuwa Mhazini Mkuu na Kibona kuwa Mhazini Msaidizi.

Ndugu Alex Temba akila kiapo kuwa Mwenyekiti Mpya wa SHIMIWI mbele ya Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja (kulia) na Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzania ambaye pia ni Wakili (kushoto)
Ndugu Alex Temba akila kiapo kuwa Naibu Katibu Mkuu Mpya wa SHIMIWI mbele ya Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja (kulia) na Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzania ambaye pia ni Wakili (kushoto)

Wajumbe waliochaguliwa Viti Maalum wanawake ni Mariam Issa Kihange na Mwajuma Issa Kissengo huku kwa upande wa wajumbe wa kawaida nafasi hizo zilichukuliwa na  Damian Manembe, Alois Matthew Ngonyani, Apollo Damian Kayungi, Assumpta Mwilanga na Selemani Kifyoga.

Ndugu Mwajuma Kissengo akila kiapo kuwa Mwenyekiti Mpya wa SHIMIWI mbele ya Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja (kulia) na Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzania ambaye pia ni Wakili (kushoto)
Bi. Mwajuma Kissengo akila kiapo kuwa Mjumbe wa viti Maalum Mpya wa SHIMIWI mbele ya Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja (kulia) na Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzania ambaye pia ni Wakili (kushoto)

Aidha uongozi huo utadumu madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI).

Wajumbe wakiwa katika zoezi la upigaji kura uchaguzi wa SHIMIWI Mkoani Morogoro
Wajumbe wakiwa katika zoezi la upigaji kura uchaguzi wa SHIMIWI Mkoani Morogoro

Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja ameupongeza uongozi mpya na kuutaka uongozi huo kubadilisha katiba ya Shirikisho hilo ndani ya miezi mitatu kuhakikisha kwamba wanatoa nafasi ya wajumbe kila mmoja awe na kazi yake na kuwa na kitengo maalum cha kutunza kumbukumbu kwa ajili ya kuweka historia ya SHIMIWI.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiupongeza uongozi mpya wa SHIMIWI baada ya Uchaguzi Mkoani Morogoro
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiupongeza uongozi mpya wa SHIMIWI baada ya Uchaguzi Mkoani Morogoro

“Napenda kuupongeza sana uongozi mpya uliochaguliwa kuingia madarakani, ila tu niwaombe mbadilishe katiba ya Shirikisho ili kuhakikisha kwamba mnatoa nafasi ya wajumbe kila mmoja awe na kazi yake na kuwa na kitengo maalum cha kutunza kumbukumbu kwa ajili ya kuweka historia ya SHIMIWI,”Alisema Kiganja.

Nae Mwenyekiti wa SHIMIWI Ndugu Daniel Mwalusamba ameushukuru uongozi wa BMT kwa kusimamia vyema uchaguzi huo na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Baraza sambamba na kuwataka viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa shughuli za SHIMIWI zinasimamiwa na kuendelezwa ipasavyo.

Mwenyekiti wa SHIMIWI Daniel Mwalusamba ameushukuru uongozi wa BMT kwa kusimamia vyema uchaguzi huo na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Baraza
Mwenyekiti wa SHIMIWI Daniel Mwalusamba akiushukuru uongozi wa BMT kwa kusimamia vyema uchaguzi huo na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Baraza

“Naushukuru sana Uongozi wa BMT kwa kusimamia vyema uchaguzi na Kuahidi kutekeleza maelekezo yote tuliyopewa na Baraza na niwaombe viongozi wote mliochaguliwa kufanya kazi kwa bidiii ili kuhakikisha kuwa shughuli za SHIMIWI zinasimamiwa na kuendelezwa ipasavyo,”Alisema Mwalusamba.

155 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2017/12/18/mwalusamba-kuliongoza-shimiwi-kwa-awamu-nyingine-tena/">
RSS