WATUMISHI WA BMT WAASWA KUVISIMAMIA VYAMA VYA MICHEZO KWA KUFUATA SHERIA, KANUNI NA KATIBA ZAO.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Susan Mlawi akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Katibu wa BMT
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Suzan Mlawi akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Katibu wa BMT

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi Suzan Mlawi amewaasa Watumishi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuvisimamia vyama vya Michezo nchini kwa kufuata Sheria Kanuni na Katiba zao ili kuhakikisha vinasimama imara na kueleta maendeleo ya Michezo nchini.

Bi Suzan ameyasema hayo wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo ya Serikali yenye ofisi zake  Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tarehe 10 Januari 2018, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika Taasisi za Wizara hiyo baada ya kuteuliwa kwake.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Susan Mlawi akiwa katika moja ya Ofisi za BMT
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Suzan Mlawi akiwa katika moja ya Ofisi za BMT

“Naomba simamieni sheria,kanuni na katiba za vyama vya Michezo ili kuhakikisha vinasimama imara na kuleta maendeleo ya Michezo nchini,”Alisema Bi Suzan Mlawi.

IMG_0089

Aidha amemtaka msajili wa vyama vya Michezo bwana Ibrahim Sapi Mkwawa kuvisimamia vyama kwa kufanya ufuatiliaji na kutathmini kama vyama vilivyopo vinakidhi vigezo vya kusimamia Michezo na kuleta maendeleo michezoni.

IMG_0078

Lakini pia amewataka Watumishi wa BMT kufanya kazi kwa pamoja, kushirikiana na kwa amani.

Katibu wa BMT Mohammed Kiganja akielezea ni kwa jinsi gani Baraza la Michezo litatekeleza maagizo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Susan Mlawi
Katibu wa BMT Mohammed Kiganja akielezea ni kwa jinsi gani Baraza la Michezo litatekeleza maagizo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Susan Mlawi

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja amemuhakikishia Katibu Mkuu wa Wizara kuyatekeleza maagizo yake kwa wakati na kwa ufasaha ili kuliimarisha Baraza katika utendaji kazi zake.

42 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/01/11/watumishi-wa-bmt-waaswa-kuvisimamia-vyama-vya-michezo-kwa-kufuata-sheria-kanuni-na-katiba-zao/">
RSS