TAMKO LA SERIKALI KUHUSU USHIRIKI WA ALPHONCE SIMBU KATIKA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA

Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari akizungumzia suala la Simbu kutoshiriki katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola
Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari akizungumzia suala la Simbu kutoshiriki katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola

Serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT) imetoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa mwanariadha Alphonce Felix Simbu katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika Gold Coast nchini Australia mwezi Aprili Mwaka 2018, kwani kuwekuwepo na sintofahamu na taarifa mbalimbali kwa umma kuhusu mwanariadha huyo kugomea kushiriki mashindano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu suala hilo Januari 17 2018, Afisa habari wa BMT Bi Najaha Bakari amesema ukweli wa suala hilo ni kwamba mshindi huyo wa tatu katika mashindano ya kimataifa ya riadha ya London mwaka 2017, ameomba kutoshiriki katika mashindano ya Jumuiya ya Madola ya mwaka huu ili apate nafasi kushiriki kwenye mashindano ya London Marathon yanayotarajiwa kufanyika mwezi Aprili 2018 na kujiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo,Japan mwaka 2020.

“ukweli ni kwamba Simbu ameomba kutoshiriki katika mashindano ya Jumuiya ya Madola ya mwaka huu ili apate nafasi ya kushiriki kwenye mashindano ya London Marathon yanayotarajiwa kufanyika mwezi Aprili 2018 na kujiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo, Japan Mwaka 2020,”Alisema Najaha.

Mashindano ya London atakayoshiriki ni moja kati ya mashindano makubwa ya riadha yanayoshirikisha wanariadha mahili duniani.Hii ni fursa kubwa kwa Simbu kuitangaza nchi yetu lakini vilevile kufungua fursa kwa wanariadha wengine wa Tanzania kushiriki katika mashindano hayo makubwa.

Aidha Bi Najaha amesema Serikali kwa kushirikiana na chama cha riadha Tanzania (RT) na kamati ya olimpiki Tanzania (TOC) katika kikao walichoketi Tarehe 13 Januari 2018 wameridhia ombi hilo ili mwanariadha huyo apate muda wa kutosha kujiandaa na kuweza kuliwakilisha vyema Taifa katika mashindano hayo ya London.

Kwa upande mwingine amewaondoa hofu watanzania kuhusu mashindano ya Jumuiya ya Madola kwani bado nchi ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa kuwa kuna vijana wengi ambao wameandaliwa na wamekidhi vigezo vya kushiriki katika mashindano hayo.

 

221 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/01/18/tamko-la-serikali-kuhusu-ushiriki-wa-alphonce-simbu-katika-mashindano-ya-jumuiya-ya-madola/">
RSS