MASHINDANO YA UMISSETA NA UMITASHUMTA NDIYO CHIMBUKO LA WACHEZAJI WENGI NCHINI.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi na BMT katika karakana ya kuchapisha magazeti ya Mwananchi
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Oliver Albert na Imani Makongoro na BMT Bw. Joseph na Bi.Bahati Msofe katika karakana ya kuchapisha magazeti ya Mwananchi

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohamed Kiganja ameipongeza kampuni ya Mwananchi kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Nyanja ya Michezo kwani wamekuwa msaada mkubwa katika michuano mbalimbali kama vile ya Ndondo Cup, hivyo basi kuiomba kampuni hiyo kuitazama na kutoa msaada katika michezo ya Umisseta pamoja na umitashumta ambayo ndio chimbuko kubwa la wachezaji wengi wanaojulikana hapa nchini.

Katibu Kiganja ameyasema hayo Januari 30 mwaka 2018, alipotembelea ofisi za Mwananchi inayojishughulisha na uchapishaji wa magazeti ya Habari mbalimbali za kijamii pamoja na Habari za michezo iliyopo maeneo ya Tabata Relini Jijini Dar es salaam na kushuhudia jinsi ofisi hiyo inavyofanya kazi katika maeneo mbalimbali.

Kiongozi wa karakana ya Mwananchi Eugen Collin (mwenye Fulana ya Bluu-bahari) akielezea jinsi mashine na mfumo mzima wa mitambo ya Kuchapisha magazeti unavyofanya kazi.
Kiongozi wa karakana ya Mwananchi Eugen Collin (mwenye Fulana ya Bluu-bahari) akielezea jinsi mashine na mfumo mzima wa mitambo ya Kuchapisha magazeti unavyofanya kazi.

“Niwapongeze sana kampuni ya Mwananchi kwa kazi nzuri mnayofanya katika Tasnia ya michezo kwani umekuwa mkitoa msaada katika mashindano mbalimbali kama vile michuano ya Ndondo Cup, lakini niwaombe pia kuangalia mashindano yanayokuza vijana hapa nchini kama vile Umisseta pamoja na Umitashumta kwani ndio chimbuko la wachezaji wengi hapa nchini,”Alisema Kiganja.

Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja(mwenye Suti) akizungumza na Mhariri wa gazeti la Mwananchi Mambo ya Jamii Ndugu Ndimara Tegambwage(aliyevaa Kofia)
Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja(mwenye Suti) akizungumza na Mhariri wa gazeti la Mwananchi Mambo ya Jamii Ndugu Ndimara Tegambwage(aliyevaa Kofia)

Aidha Katibu Kiganja amewasihii viongozi wa Kampuni ya Mwananchi kuendelea kuwapa mafunzo ya kila mara waandishi na wafanyakazi wa Kampuni hiyo kuhusu masuala ya Habari za Jamii pamoja na Michezo ili kuendelea kuboresha kazi wanazozifanya na kuzitoa kila siku.

 

83 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/01/30/mashindano-ya-umisseta-na-umitashumta-ndiyo-chimbuko-la-wachezaji-wengi-nchini/">
RSS