WAZIRI MWAKYEMBE AKABIDHIWA RASIMU YA KATIBA YA CHOMBO CHA KUSIMAMIA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe (Aliyevaa suti) akikabidhiwa Rasimu ya katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania na mwenyekiti wa kamati hiyo Ndugu Emmanuel Saleh (kushoto) na katikati ni Katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe (Aliyevaa suti) akikabidhiwa Rasimu ya katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania na mwenyekiti wa kamati hiyo Ndugu Emmanuel Saleh (kushoto) na katikati ni Katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja.

Kamati ya wajumbe kumi na tatu wa kuunda katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa iliyoundwa na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe miezi miwili iliyopita, imekabidhi Rasimu ya katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania.

Akikabidhi Rasimu hiyo kwa Mheshimiwa Mwakyembe Jumamosi ya tarehe 3 Februari 2018 katika moja ya kumbi za Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndugu Emmanuel Saleh amemshukuru Mheshimiwa Waziri kwa jitihada alizozifanya za kuleta Amani, Mshikamano na Maendeleo kwenye sekta ya Michezo hasa katika mchezo wa masumbwi licha ya kuwepo kwa migogoro, lakini aliona umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti za kutatua migogoro hiyo iliyodumu kwa muda mrefu katika mchezo wa ngumi za kulipwa Tanzania.

Aidha Ndugu Saleh alisema kamati hiyo ambayo ilihusisha pia watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa pamoja na Msajili wa Vyama na vilabu vya Michezo nchini, ilipewa hadidu za rejea ili kuwaongoza katika utekelezaji wa kazi yao. Hadidu hizo ni:-

  1. Kupitia na kuhuisha maoni ya katiba zilizopendekezwa na kamati iliyoundwa tarehe 6 April, 2016.
  2. Kuratibu na kukusanya maoni ya wadau.
  3. Kupitia na kukusanya usahihi na ulinganifu wa katiba za nchi mbalimbali.
  4. Kutathmini na kuchambua machapisho mbalimbali yaliyoandikwa ndani na nje ya nchi.
  5. Kuandaa rasimu ya katiba ya chombo kitakachosimamia mchezo wa ngumi za kulipwa.
  6. Kuwasilisha rasimu ya katiba kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ifikapo tarehe 31 Januari, 2018.

Kamati ilianza kazi yake mara moja na kufanikiwa kuwafikia zaidi ya wadau wa ngumi za kulipwa 200 kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo mkoa wa Dar es salaam, Pwani, Tanga, Ruvuma, Mbeya na Mtwara. Wajumbe wa kamati walitembea katika baadhi ya mikoa iliyotajwa na kukutana na wadau moja kwa moja na wengine waliwasilisha maoni yao kwa njia ya maandishi na sauti.

Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhiwa hati ya shukrani kwa kuchangia kuandaa pambano la Bondia Ibrahim Class kutoka Jo Gym na Yahya Poli (kushoto) katikati ni Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja

Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhiwa hati ya shukrani kwa kuchangia kuandaa pambano la Bondia Ibrahim Class kutoka Jo Gym na Yahya Poli (kushoto) katikati ni Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja

Ata hivyo Ndugu Saleh alisema Rasimu hiyo inabeba maono ya kuhakikisha mchezo wa ngumi za kulipwa unarejea katika enzi na hadhi yake na zaidi kutoa fursa ya vijana kujiajiri na kujiletea maendeleo wao binafsi, Jamii na nchi kwa ujumla pamoja na kulitangaza Taifa nje ya mipaka na kuwa na mabondia mahiri sana na wenye ari na moyo isipokuwa migogoro hii ndio imesababisha nchi kupoteza sifa za ubingwa kwa mikanda mbalimbali ya dunia ambapo vijana wetu wamekuwa wakipigwa kila wanapocheza nje ya Tanzania.

“Rasimu hii inabeba maono ya kuhakikisha mchezo wa ngumi za kulipwa unarejea katika enzi na hadhi yake sanjari na kutoa fursa ya vijana kujiajiri na kujiletea maendeleo wao binafsi, jamii na nchi kwa Ujumla,”Alisema Saleh.

Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison Mwakyembe akipongeza kamati iliyotengeneza Rasimu ya katiba ya chombo cha ngumi za kulipwa Tanzania, pembeni kulia ni msajili wa vyama na vilabu vya michezo Tanzania.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison Mwakyembe akipongeza kamati iliyotengeneza Rasimu ya katiba ya chombo cha ngumi za kulipwa Tanzania, pembeni kulia ni msajili wa vyama na vilabu vya michezo Tanzania.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe ameipongeza kamati hiyo kwa kujitoa kuifanya kazi hiyo kwa umahiri mkubwa na inaonyesha ni jinsi gani wadau hao wa masumbwi nchini wamechoka kwa migogoro ambayo imekuwa ikiendelea katika mchezo wa ngumi nchini.

“Niwapongeze sana kwa kujitoa kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja na kwa umahiri mkubwa kuhakikisha kuwa tunapata rasimu kwa wakati, mmejitolea pesa zenu wenyewe kuzunguka katika baadhi ya mikoa kukusanya maoni ya wadau wa ngumi, na hii inaonyesha ni jinsi gani mmechoka kwa migogoro ambayo imekuwa ikiendelea katika mchezo wa ngumi nchini,”Alisema Mhe. Mwakyembe.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja (Katikati) akikabidhiwa hati ya shukrani na Yahya Poli kutoka Jo Gym kwa kuchangia katika pambano la Ngumi la Kimataifa la Ibrahim Class lililofanyika Tarehe 25 Novemba 2017.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja (Katikati) akikabidhiwa hati ya shukrani na Yahya Poli kutoka Jo Gym kwa kuchangia katika pambano la Ngumi la Kimataifa la Ibrahim Class lililofanyika Tarehe 25 Novemba 2017, kulia ni Mh. Mwakyembe akishuhudia tukio hilo.

31 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/03/waziri-mwakyembe-akabidhiwa-rasimu-ya-katiba-ya-chombo-cha-kusimamia-ngumi-za-kulipwa-nchini/">
RSS