BMT LATANGAZA KAMATI YA KUSIMAMIA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI ILIYOTEULIWA NA MH. MWAKYEMBE

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe (Aliyevaa suti) akikabidhiwa Rasimu ya katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania na mwenyekiti wa kamati hiyo Ndugu Emmanuel Saleh (kushoto) na katikati ni Katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja. Hii ilikuwa ni Februari 3, 2018
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe (Aliyevaa suti) akikabidhiwa Rasimu ya katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania na mwenyekiti wa kamati hiyo Ndugu Emmanuel Saleh (kushoto) na katikati ni Katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja. Hii ilikuwa ni Februari 3, 2018

Baraza la Michezo la Taifa BMT, Leo Februari 8, 2018, limetangaza kamati iliyoteuliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe ya kusimamia Chombo cha Ngumi za kulipwa Tanzania ambayo inaanza kazi punde tu baada ya kutangazwa.

Akitangaza kamati hiyo katika moja ya kumbi za Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa BMT Mohammed Kiganja amesema Baada ya Mheshimiwa Waziri kuipokea Rasimu ya katiba ya chombo cha kusimamia Ngumi za kulipwa nchini Tanzania, aliipongeza na kuishukuru kamati hiyo kwa kazi nzuri iliyofanya kwa umahiri mkubwa na kujitoa kwa muda wao binafsi, hivyo na kuamua kamati hiyo iendelee kusimamia Ngumi kwa kipindi hiki cha mpito.

Kamati hiyo ambayo ameiteua Mheshimiwa Waziri inajumuisha wajumbe wafuatao:-

 1. Emmanuel Saleh                                                        Mwenyekiti,
 2. Joe Anea                                                                       Makamu Mwenyekiti,
 3. Yahya Poli                                                                    Katibu,
 4. Habib Kinyogoli                                                          Mjumbe,
 5. Rashid Matumla                                                         Mjumbe,
 6. Anthony Ruta                                                              Mjumbe,
 7. Shomari Kimbau                                                         Mjumbe,
 8. Killaga M.Killaga                                                        Mjumbe,
 9. Karama Nyilawila                                                       Mjumbe,
 10. Fike Wilson                                                                  Mjumbe,
 11. Jaffar Ndame                                                               Mjumbe,
 12. Ali C. Bakari                                                                 Mjumbe,

Aidha katibu Kiganja amesema Kamati hiyo itakuwa na Majukumu yafuatayo:-

 1. Kusaidia Baraza la Michezo la Taifa Kuratibu shughuli za kila siku za Ngumi za Kulipwa Nchini Tanzania.
 2. Kupokea maoni kwa maandishi kutoka kwa wadau wa ngumi katika kipindi cha mwezi mmoja kupitia tovuti ya Baraza la Michezo la Taifa ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz na tovuti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo www.habari.go.tz
 3. Kuratibu mkutano wa kujadili Rasimu katika kipindi cha miezi miwili ili kuwapa wadau waliokosa nafasi kwa njia ya maandishi kutoa maoni yao.
 4. Kuandaa mkutano mkuu wa uchaguzi.

 

 

 

137 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/08/bmt-latangaza-kamati-ya-kusimamia-ngumi-za-kulipwa-nchini-iliyoteuliwa-na-mh-mwakyembe/">
RSS