KIGANJA: KUWENI SEHEMU YA MAENDELEO YA MICHEZO BADALA YAKUWA SEHEMU YA KUSEMEA MIGOGORO YA VYAMA VYA MICHEZO.

Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Stesheni ya Habari ya ITV Bw.Kongi Macharia kuhusu uendeshaji wa stesheni hiyo wakiwa moja studio ya Vituo vya habari vya IPP.
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Stesheni ya Habari ya ITV Bw.Kongi Macharia kuhusu uendeshaji wa stesheni hiyo wakiwa moja studio ya Vituo vya habari vya IPP.

Katibu wa Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja amevitaka vyombo vya habari kuwa sehemu ya maendeleo ya michezo nchini na kuepuka kuwa sehemu ya kusemea migogoro inayotoka  kwenye vyama vya  michezo.

Hayo ameyasema tarehe  07 Februari, 2018 katika ziara yake aliyoifanya katika vyombo vya habari vya IPP na kuongelea mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Michezo nchini, ambapo, alimalizia ziara yake kwa kushiriki kipindi maalum kilichoandaliwa na  Runinga ya TV 1 kilichohusu “Kucheweshwa kwa kalenda za matukio ya mwaka kwa vyama vya michezo na hatua zinazochukuliwa na BMT kwa vyama vinavyokaidi kuleta kalenda hizo.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja (aliyekaa) akiwa katika moja ya studio na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka Mhariri wa Michezo Amri Masare wa mwisho kulia.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja (aliyekaa) akiwa katika moja ya studio na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka Mhariri wa Michezo Amri Masare wa mwisho kulia.

Aliendelea kuwa, vyombo ya habari visikubali kupokea mtu au watu wanaotaka kupeleka migogoro ya michezo kwao badala yake wawaelekeze kufuata ngazi husika za kisheria katika kutatua migogoro yao ili kupiga hatua katika maendeleo ya michezo.

“Vyombo vya habari msikubali kupokea mtu au watu waotaka kuleta migogoro yao kwenu bali waelezeni wafuate ngazi husika kutatua migogogoro yao”Alisisitiza Kiganja”.

Hata hivyo amevitaka vyama vya michezo kufuata Sheria na Kanuni zinazoendesha michezo nchini pamoja na Katiba zao  kwani hivyo ndivyo vitatupeleka katika maendeleo ya michezo.

Katika hatua nyingine wakati wa kipindi maalum katika kituo cha Runinga cha TV 1 katika mada iliyohusu uwasilishwaji wa kalenda za matukio ya mwaka kwa  vyama Katibu wa Baraza alivitaka vyama vya michezo kuleta kalenda mapema na wasilazimishe BMT kuchukua hatua zilizopo kwenye sheria na kanuni zinazoliongoza.

Katibu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja alisema kuwa anaongeza muda wa kuleta kalenda hizo mpaka tarehe 28 mwezi huu kila chama kihakikishe kimeleta ili baraza liweze kuandaa kalenda ya matokio ya mwaka kwa vyama vyote.

Aidha, Kiganja ameeleza kuwa, ataendelea kutumia vyombo vya habari kwani ni wadau wakubwa wa maendeleo ya michezo na kutoa wito kwao kuendelea kuwa karibu na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na vyama vya michezo katika kuleta maendeleo ya michezo nchini.

Lakini pia kutangaza michezo yote na hasa kushiriki katika maandalizi ya mashindano ya michezo ya shule za Msingi (UMITASHUMTA) na shule za Sekondari (UMISSETA) kwa kuonyesha moja kwa moja mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Jijini Mwanza mwezi June mwaka huu ambayo ndiyo inayoibua vipaji na hatimaye kuleta nyota wengi wanaolitangaza Taifa.

63 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/08/kiganja-kuweni-sehemu-ya-maendeleo-ya-michezo-badala-yakuwa-sehemu-ya-kusemea-migogoro-ya-vyama-vya-michezo/">
RSS