LEODGER CHILLA TENGA KULIONGOZA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA

MWAKYEMBE(1)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe akitaja majina ya Wajumbe watakaounda Baraza la Michezo la Taifa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ikisomwa na muundo wa shughuli za Baraza, amemteua Bw. Leodger Chilla Tenga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa.

Dokta Mwakyembe pia amewateua wajumbe wengine sita (6) wa Baraza hilo kama ifuatavyo:

  1. Prof. Mkumbwa M.A. Mtambo
  2. Bi. Beatrice Singano
  3. Kanali Mstaafu Juma Ikangaa
  4. Bw. John Joseph Ndumbaro
  5. Bi. Rehema Sefu Madenge
  6. Bw. Salmin Kaniki

Aidha, Dkt. Mwakyembe amewateua wajumbe wengine watatu (3) wa Baraza kutokana na nafasi za vyeo vyao ambao ni:

  1. Yusuph Singo – Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  2. Dkt. Edicome Shirima – kamishna wa Elimu , Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.
  3. Mohammed Kiganja, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa ambaye atakuwa ni Katibu wa Baraza.

Uteuzi wajumbe wote umeanza rasmi tarehe 08 Februari,2018 na watalitumikia Baraza kwa kipindi cha Miaka Mitatu (3).

vilevile Dkt. Mwakyembe kwa mujibu wa sheria amemteua Bw. Timothy Mganga kuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kwa kipindi cha miaka mitano (5)

49 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/09/leodger-chilla-tenga-kuliongoza-baraza-la-michezo-la-taifa/">
RSS