DKT. MWAKYEMBE AWATAKA WAHARIRI KUJIPANGA UJIO WA VIONGOZI WA FIFA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na Wahariri na Waandishi wa habari za Michezo katika kikao chake ikiwa ni maandalizi ya ujio wa ugeni mkubwa katika sekta ya soka nchini Rais wa FIFA, CAF na ujumbe wake kutoka nchi 25, kulia ni Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Yusuph Singo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na Wahariri na Waandishi wa habari za Michezo katika kikao chake Februari 13, 2018 ikiwa ni maandalizi ya ujio wa ugeni mkubwa katika sekta ya soka nchini Rais wa FIFA, CAF na ujumbe wake kutoka nchi 25, kulia ni Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Yusuph Singo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison  Mwakyembe amewataka wahariri na Waandishi wa Habari na Michezo kujipanga kupokea ujio wa viongozi wakubwa katika soka kutoka FIFA ambao wanakuja katika vikao vyao mwisho wa mwezi huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza jana katika kikao na wahariri wa habari za michezo  Waziri  Mwakyembe alisema kuwa mnamo  Februari 20-23 Rais wa FIFA, Rais wa CAF pamoja na Marais  mbalimbali wa soka  kutoka katika nchi zaidi ya 21 duniani wanatarajiwa kuja nchini wakitokea nchini Nigeria kushiriki vikao vyao vya FIFA, ambapo Tanzania ni mwenyeji wa vikao hivyo vya soka kidunia katika awamu hii.

Hata hivyo ameitaka mitandao ya kijamii kuandika vitu ambayo vitakuwa vinazungumzwa na kuacha kuandika vitu tofauti na kikao hicho ambapo itapelekea kuichafua nchi na kusababisha kukosa fursa nyingi za maendeleo ya michezo na hasa soka ambayo ndio kikao chao.

‘’Unajua mitandao na media zipo nyingi na wengine wamekuwa wapo katika kufanya machafuzi hivyo naomba tuonyeshe ushirikiano zaidi katika kikao hicho na kuondoa tofauti zetu ili kuweza kufanikiwa na fursa zinazotokana na Ujio huo’’alisema.

Aliongeza kuwa hatopenda yatokee kama yaliyotokea kipindi cha ujio wa Evarton ambapo waandishi wengi walifungiwa nje ni bora kujipanga mapema tuepuke aibu hiyo.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leodger Tenga (katikati)akizungumza na wahariri pamoja na  waandishi wa vyombo vya habari juu ya ujio wa Viongozi wa Fifa na Caf(kushoto ) Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe huku kulia ni Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Yusuph Singo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leodger Tenga (katikati)akizungumza na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo vya habari juu ya ujio wa Viongozi wa Fifa na Caf(kushoto ) Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe huku kulia ni Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Yusuph Singo.

Mwenyekiti Mpya wa Baraza la michezo la Taifa Leodigar Chilla Tenga  alisema kuwa  tumejipanga kupokea wageni hao ambao wanakuja katika kikao  hicho akiwemo Rais wa FIFA Pamoja na wa CAF.

Aliongeza kuwa nchi yetu haijawahi kutembelewa na viongozi hao ambao wanakuja kufanya semina yao, ambapo, kutakuwa na viongozi wengine Marais na Makatibu wa Michezo duniani kutoka karibu nchi zaidi ya 21.

‘’Ni wakati wa kufurahia ujio huo kwani viongozi hao ni wasimamizi  katika soka na wafadhiri wakubwa katika kuongeza maendeleo  michezo hivyo, ningependa waondoke hapa na sifa za kutosha na  kujenga  sifa kwa wakuu hao ili wajione kuwa wametembea katika nchi ya soka’’alisema na kuongeza kuwa;

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakimsikiliza waziri wa habari utamaduni sanaa na Michezo katika kikao kilichofanyika juzi katika ukumbi wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakimsikiliza waziri wa habari utamaduni sanaa na Michezo katika kikao kilichofanyika juzi katika ukumbi wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Kuonyesha ukarimu pindi wageni wakiwa nchini  kunaweza kuleta maendeleo katika soka kwa kuwa ni viongozi wanaopenda maendeleo zaidi.

‘’Nafikiri mnakumbuka kuwa wameondoa  msaada wa maendeleo ambao ulikuwa  dola milioni 1.5 mpaka milioni 5 kwa miaka minne na hili sio jambo dogo mpaka wamefiki kufanya hivyo na kufikiria kuja Tanzania na Nigeria kuna sababu zao kwa sababu wameona watanzania wanapenda  Soka na Wanaenda sawa na ajenda zao, pia ujio huo unaashiria jinsi gani wageni hao wanapenda kuona mpira wa wanawake unavyoendelea na vijana pamoja na Uadilifu ’’alisema.

Alifafanua kuwa lengo la kikao chao ni pamoja kupanga maendeleo, jinsi gani kufanikisha kuendeleza soka na kusaidia kufikia malengo ya kufikisha soka katika kiwango.

27 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/14/dkt-mwakyembe-awataka-wahariri-kujipanga-ujio-wa-viongozi-wa-fifa/">
RSS