MWAKYEMBE: TFF SIMAMENI IMARA KUHAKIKISHA AFCON U17 2019 INAFANA.

Kamati ya maandalizi ya Afcon U17 2019, ikiongozwa na Mheshimiwa Mwakyembe kama mwenyekiti, Leodger Tenga (makamu mwenyekiti), Henry Tandau (katibu), pamoja na wajumbe wengine Yusuph Singo (aliyesimama), Mohammed Kiganja (aliyekaa baada ya Yusuph Singo upande wa kulia) Warace Karia (aliyekaa upande wa kushoto baada Leodger Tenga).
Kamati ya maandalizi ya Afcon U17 2019, ikiongozwa na Mheshimiwa Mwakyembe kama mwenyekiti, Leodger Tenga (makamu mwenyekiti), Henry Tandau (katibu), pamoja na wajumbe wengine Yusuph Singo (aliyesimama), Mohammed Kiganja (aliyekaa baada ya Yusuph Singo upande wa kulia) Warace Karia (aliyekaa upande wa kushoto baada Leodger Tenga).

Kamati ya maandalizi ya michuano ya kombe la mataifa Barani Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, imekutana Februari 14, 2018 kujadili maendeleo ya maandalizi hayo kuhakikisha kuwa Tanzania inafanya vyema kama mwenyeji katika michuano hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika hotel ya Courtyard Protea jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa kamati hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harisson Mwakyembe amesema inatia moyo kuona kamati hiyo inaendelea vizuri na maandalizi ya michuano hiyo mikubwa inayotarajiwa kufanyika nchini mwaka 2019.

“kiukweli inatia moyo kuona tumepiga hatua katika maandalizi ya Afcon U17 2019, licha ya kuwepo changamoto za hapa na pale lakini ni lazima tuitumie fursa tuliyopewa vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri kama wenyeji katika michuano hiyo,”Alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha Mheshimiwa Mwakyembe amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, kusimama imara kuhakikisha michuano hiyo inafana bila kuwa na dosari yoyote ili kuweza kulishawishi shirikisho la mpira wa miguu Barani Afrika CAF na Duniani FIFA kuipa nafasi Tanzania kuandaa mashindano mengine makubwa siku za usoni.

Tanzania itaandaa Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, baada ya kukabidhiwa uenyeji na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika hafla mwaka jana nchini Gabon, ambapo hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuandaa fainali hizo za soka Afrika tofauti na mataifa mengine kama vile Rwanda, Ghana, Nigeria, Afrika Kusini, Misri na Angola ambayo yameandaa mara kadhaa Mashindano hayo.

68 total views, 3 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/15/mwakyembe-tff-simameni-imara-kuhakikisha-afcon-u17-2019-inafana/">
RSS