DOKTA NASSORO ALLY MATUZYA AFUNGIWA KUJISHUGHULISHA NA SHUGHULI ZA UONGOZI WA CHAMA CHA MADAKTARI WA MICHEZO (TASMA) KWA MIAKA MITATU

Kaimu Msajili wa Vilabu na Vyama vya Michezo Nchini Ibrahim Sapi Mkwawa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kufungiwa kwa Dokta Nassoro Matuzya.
Kaimu Msajili wa Vilabu na Vyama vya Michezo Nchini Ibrahim Sapi Mkwawa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kufungiwa kwa Dokta Nassoro Matuzya.

Ofisi ya Msajili wa vyama na vilabu vya Michezo nchini, chini ya Baraza la Michezo la Taifa BMT, kupitia Kaimu Msajili Ibrahim Sapi Mkwawa imemfuta na kumfungia Ndugu Nassoro Ally Matuzya kujishughulisha na shughuli za uongozi wa chama cha madaktari wa Michezo (TASMA) kuanzia Tarehe 15 Februari, 2018.

Bw. Mkwawa amesema Mnamo Tarehe 11 Oktoba, 2017 kwa kutumia mamlaka aliyopewa na kifungu cha 20(3) cha sheria ya BMT ya 1967, kama iliyorekebishwa 1971 aliagiza kufanyika ukaguzi wa akaunti za TASMA kufuatia malalamiko yaliyoletwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho. Baada ya ukaguzi huo ilibainika kuwa chama kinaendesha shughuli zake bila ya kuwa na akaunti kufuatia kufungwa kwa akaunti Namba 01J1027507900 iliyopo CRDB Benk.

Kwa mujibu wa katiba ya TASMA Katibu mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kutayarisha ripoti ya fedha kwa kusaidiana na Mhazini, kitendo cha kufungwa kwa akaunti ya chama ni ukiukwaji wa ibara ya 38 (6) (7) na 48 ya katiba ya TASMA.

Aidha imebainika kuwa kutokana na kutokuwepo kwa akaunti inayotambulika ya chama, fedha zilizokuwa zinapatikana zilikuwa zinakusanywa moja kwa moja na Katibu Mkuu (Dr. Nassoro Matuzya) na haziendi kwenye chama.

Hivyo basi, kwa mamlaka aliyopewa na kanuni ya 10(1) (b) na (c) amemfuta uongozi kwa kipindi kilichobakia na vile vile kumfungia kujishughulisha na shughuli za uongozi wa chama chochote cha Michezo nchini kwa kipindi cha miaka mitatu.

173 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/19/dokta-nassoro-ally-matuzya-afungiwa-kujishughulisha-na-shughuli-za-uongozi-wa-chama-cha-madaktari-wa-michezo-tasma-kwa-miaka-mitatu/">
RSS