BMT LAAGIZA ADA ZA ZAMANI ZIENDELEE KUTUMIKA KATIKA KUANDAA MBIO ZA MARATHON

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maelekezo ya Serikali Juu ya Ada Mpya za waandaaji wa mbio za Marathon
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maelekezo ya Serikali Juu ya Ada Mpya za waandaaji wa mbio za Marathon

Serikali kupitia katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja imeagiza ada za zamani ziendelee kutumika katika kuandaa mbio hizo kwa sasa mpaka Serikali itakapotoa maelekezo katika kikao kitakachofanyika kati ya BMT, RT na waandaaji wa mbio hizo tarehe 5 Machi Mkoani Kilimanjaro mara baada ya mashindano ya mwaka huu kumalizika.

Katibu Kiganja amesema Kufuatia malalamiko yanayotolewa na waandaaji wa mbio za marathon juu ya kupandishwa kwa kiwango cha ada ya kuendesha mbio hizo, kupitia kikao kilichokaliwa tarehe 07 Oktoba 2017, kati ya msajili, uongozi wa RT na wadau wa mashindano hayo.

“Kufuatia malalamiko yanayotolewa na waandaaji wa mbio za marathon juu ya kupandishwa kwa kiwango cha ada ya kuendesha mbio hizo, kupitia kikao kilichokaliwa tarehe 07 Oktoba 2017, kati ya msajili, uongozi wa RT na wadau wa mashindano hayo,”Alisema Kiganja.

Kwa mujibu wa uongozi wa RT wamezitenga mbio hizo katika ngazi tofauti za ada ambapo kwa sasa ada kubwa ni kuanzia milioni 6 kwa mbio ndefu ambapo zamani ada ilikuwa ni milioni 2, na mbio fupi kwa sasa ni kuanzia milioni 4 hadi milioni 2 pamoja na ada za chama cha riadha  katika Mkoa mashindano yanapofanyikia ambapo zamani mbio fupi ada ilikuwa ni milioni 1.

Maelekezo ya utendaji kazi wa waratibu hao ni lazima washirikiane na Kamati ya Michezo ya Mkoa husika na wawape kibali cha kazi hiyo.

Pia lazima washirikiane na chama cha riadha cha Mkoa husika, kama italazimu kupata wataalam kutoka riadha Taifa watawasiliana nao ili kwenda kutoa utaalam wao.

Aidha katibu Kiganja amesema Ikumbukwe kuwa Tarehe 16 Septemba 2017, chama cha Riadha kiliitisha kikao na wadau wake hao ili kuwekana sawa katika uendeshaji wa mbio hizo kwa kuwa ni kipindi kirefu sasa mbio za marathon zimekuwa zikiendeshwa kiholela bila kufuata utaratibu wa kuziratibu.

Katika kikao cha Oktoba 7, pamoja na mambo mengine uongozi wa RT ulifahamishwa na msajili wa vyama na vilabu vya Michezo nchini, umuhimu na ulazima wa kufuata sheria, kwa waandaaji wa mashindano ya marathon kusajiliwa kama wakuzaji na mawakala wa Michezo kwa mujibu wa kanuni ya 19 (1) (2) na (3).

151 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/20/bmt-laagiza-ada-za-zamani-ziendelee-kutumika-katika-kuandaa-mbio-za-marathon/">
RSS