BMT LAVIPONGEZA SIMBA NA YANGA KWA KUSONGA MBELE MICHUANO YA KIMATAIFA

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akivipongeza Simba na Yanga kwa kufanikiwa kusonga mbele katika Michuano ya kombe la Klabu Bingwa na Shirikisho Barani Afrika.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akivipongeza Simba na Yanga kwa kufanikiwa kusonga mbele katika Michuano ya kombe la Klabu Bingwa na Shirikisho Barani Afrika.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja amevipongeza vilabu vya Simba na Yanga kwa kufanikiwa kusonga mbele katika hatua inayofuata mashindano ya kimataifa kwa upande wa vilabu Barani Afrika.

Katibu Kiganja amesema ni vyema vilabu hivyo vikubwa vinavyowakilisha nchi katika michuano ya klabu bingwa pamoja na shirikisho Barani Afrika vikapambana kuhakikisha vinafika mbali katika michuano hiyo ili kuweza kuliletea Taifa sifa sanjari na kuwafanya wachezaji wake kuonekana kimataifa ili waweze kusajiliwa na Tanzania kuweza kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Wachezaji wa Simba wakishangilia Bao pekee lililofungwa na Okwi katika mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Gendermarie Nchini Djibouti.
Wachezaji wa Simba wakishangilia Bao pekee lililofungwa na Okwi katika mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Gendermarie Nchini Djibouti.

“Ni vyema klabu za Simba na Yanga kuhakikisha vinapambana katika michuano hii mikubwa Barani Afrika, ili kuweza kufika mbali, kuliletea taifa sifa nzuri sanjari na kuwafanya wachezaji wake kuonekana kimataifa ili waweze kusajiliwa na Tanzania kuweza kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi”Alisema Kiganja.

Timu ya St.Louis na Yanga zikiingia uwanjani katika mchezo wa marudiano kombe la klabu Bingwa Barani Afrika nchini Shelisheli
Timu ya St.Louis na Yanga zikiingia uwanjani katika mchezo wa marudiano kombe la klabu Bingwa Barani Afrika nchini Shelisheli.

Klabu ya Simba imefanikiwa kusonga mbele katika hatua inayofuata kombe la shirikisho Barani Afrika baada ya kuiyondoa klabu ya Gendermarie ya Djibouti kwa jumla ya mabao 5-0, huku klabu ya Yanga ikiing’oa klabu ya St. Louis kutoka shelisheli kwa jumla ya mabao 2-1.

43 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/21/bmt-lavipongeza-simba-na-yanga-kwa-kusonga-mbele-michuano-ya-kimataifa/">
RSS