JICA NA TaBSA KUFUNDISHA MCHEZO WA BASEBALL KATIKA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA TEMEKE

Baadhi ya wachezaji wakiwa katika mafunzo ya mchezo wa Baseball nchini Tanzania.
Baadhi ya wachezaji wakiwa katika mafunzo ya mchezo wa Baseball nchini Tanzania.

Chama cha mchezo wa Baseball and Softball nchini Tanzania (TaBSA) kwa kushirikiana na Shirika la Mashirikiano la Kimataifa la Japan (JICA) wanatarajia kuanza mafunzo ya mchezo wa Baseball kwa baadhi ya shule za msingi Wilayani Temeke kuanzia Tarehe 26 Februari hadi 15 Machi mwaka 2018.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha walimu wa kujitolea wa mchezo huo kutoka nchini Japan kwa kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha , Katibu wa Chama cha Baseball and Softball Ndugu Alpherio Nchimbi, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wanafunzi wa Shule za Msingi ili wanapokuwa na kujiunga na sekondari wawe na uelewa mkubwa wa mchezo huo na ata kufanya vizuri katika siku za usoni.

Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bi. Neema Msitha(mwenye blauzi ya Bluu katikati) akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa kujitolea kufundisha mchezo wa Baseball kutoka nchini Japan na katibu wa TaBSA Alpherio Nchimbi (mwenye shati la Kijivu).

“Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo wanafunzi wa Shule za Msingi ili wanapokuwa na kujiunga na sekondari wawe na uelewa mkubwa wa mchezo huu na ata kufanya vizuri katika siku za usoni,”Alisema Nchimbi.

Kwa upande wake kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bi.Neema Msitha amelipongeza shirika la JICA kwa kushirikiana na Chama cha TaBSA kwa kujitolea kuhakikisha kuwa mchezo wa Baseball unajulikana nchini na matumaini makubwa ni kuona mchezo huo unafanya vizuri katika medani ya kimataifa.

Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bi. Neema Msitha akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa walimu wa kujitolea kufundisha mchezo wa Baseball Kutoka nchini Japan Bw. Yoh Mizuta.
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bi. Neema Msitha akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa walimu wa kujitolea kufundisha mchezo wa Baseball Kutoka nchini Japan Bw. Yoh Mizuta.

“Ni jambo zuri sana kuona shirika la JICA kwa kushirikiana na Chama cha TaBSA kujitolea kuhakikisha kuwa mchezo wa Baseball unajulikana nchini na Matumaini yetu makubwa kama BMT ni kuona mchezo huo unafanya vizuri katika medani ya kimataifa siku za baadaye, tunatoa Baraka zote muendelee kueneza mchezo huu mashuleni kwa manufahaa ya wanafunzi, waalimu na nchi kwa ujumla,”Alisema Neema.

52 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/23/jica-na-tabsa-kufundisha-mchezo-wa-baseball-katika-baadhi-ya-shule-za-msingi-wilaya-ya-temeke/">
RSS