BMT LASITISHA UCHAGUZI BFT NA KUUNDA KAMATI YA KUONGOZA NGUMI ZA RIDHAA NCHINI

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akitangaza kamati ya wajumbe 6 itakayoongoza BFT kwa kipindi cha Miezi Mitatu.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akitangaza kamati ya wajumbe 6 itakayoongoza BFT kwa kipindi cha Miezi Mitatu.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja amesitisha uchaguzi wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa uliopangwa kufanyika tarehe 24 Februari 2018 mjini Dodoma kutokana na katiba ya Shirikisho hilo kutokidhi matakwa ya wadau wake likiwemo shirikisho la ngumi za ridhaa duniani  (AIBA).

Katibu Kiganja amesema uongozi uliopita umeshindwa kutekeleza maagizo ya kurekebisha katiba katika kipindi chote walipokuwa madarakani na kushindwa kubainisha madhumuni ya katiba hiyo, jambo ambalo lilitakiwa kufanyika kabla ya BFT kuitisha uchaguzi mwingine wa viongozi.

“Uongozi uliopita umeshindwa kutekeleza maagizo ya kurekebisha katiba katika kipindi chote walipokuwa madarakani na kushindwa kubainisha madhumuni ya katiba hiyo, jambo ambalo lilitakiwa kufanyika kabla ya BFT kuitisha uchaguzi mwingine wa viongozi,’’Alisema Kiganja.

Baadhi ya wajumbe wa Uchaguzi wa BFT, wakimsikiliza kwa umakini katibu wa BMT Mohammed Kiganja alipokuwa anasitisha Uchaguzi wa BFT mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Uchaguzi wa BFT, wakimsikiliza kwa umakini katibu wa BMT Mohammed Kiganja alipokuwa anasitisha Uchaguzi wa BFT mjini Dodoma.

Aidha Kiganja ameunda kamati ya Ngumi za Ridhaa yenye wajumbe 6 itakayosimamia masuala yote ya ngumi za ridhaa kwa kipindi cha miezi mitatu ya mpito kabla ya kufanyika uchaguzi mwingine kuwapata viongozi wapya. Kamati hiyo inaundwa na wajumbe wafuatao:

 1. Muta Rwakatare                                                                  Mwenyekiti
 2. Yono Kevela                                                                          Mjumbe
 3. Samwel Sumwa                                                                    Mjumbe
 4. Lucas Ruta                                                                            Mjumbe
 5. Aisha Veniatus                                                                     Mjumbe
 6. Mohammed Abubakari                                                      Mjumbe

Kamati hiyo itakuwa na Majukumu yafuatayo:

 1. Kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi
 2. Kurekebisha katiba ya Shirikisho
 3. Kuratibu shughuli za Shirikisho za kila siku.
 4. Kuhakikisha inawapungumzia mzigo wajumbe katika uchaguzi ujao.
 5. Kuunda kanuni za uchaguzi, kiufundi na utawala.

 

47 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/24/bmt-lasitisha-uchaguzi-bft-na-kuunda-kamati-ya-kuongoza-ngumi-za-ridhaa-nchini/">
RSS