KAMATI YA NGUMI ZA KULIPWA YAKUTANA NA MABONDIA KUPATA MAONI YAO.

Viongozi wa kamati ya ngumi za kulipwa wakiongozwa na mwenyekiti Emmanuel Saleh (katikati) Joe Anea (makamu mwenyekiti-kulia ) na ndungu Yahaya Poli- katibu (kushoto) wakiwa katika kikao na mabondia wa ngumi za kulipwa

Kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini, ikiongozwa na mwenyekiti wake ndugu Emmanuel  Saleh imeendelea kupokea maoni ya wadau wa mchezo wa ngumi, huku leo hii tarehe 28 Februari 2018 ikikutana na mabondia wa ngumi za kulipwa katika ukumbi wa uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Katika mkutano huo mwenyekiti wa kamati Bw. Saleh aliwataka mabondia kuwa huru katika kujenga hoja za msingi ambazo zitaweza kuwaweka mabondia katika hali nzuri kimaisha katika siku za usoni sanjari na kuweka historia katika mapambano ya ngumi kimataifa.

Baadhi ya mabondia wa ngumi za kulipwa nchini wakitoa maoni yao kwa kamati ya ngumi za kulipwa kuhusu mchezo wa ngumi.
Baadhi ya mabondia wa ngumi za kulipwa nchini wakitoa maoni yao kwa kamati ya ngumi za kulipwa kuhusu mchezo wa ngumi.

“Nataka muwe huru na kujenga hoja za msingi ambazo zitaweza kuwasaidia na kuwaweka katika hali nzuri kimaisha katika siku za usoni pamoja na kuweka historia katika mapambano ya ngumi kimataifa,”Alisema Saleh.

Aidha kwa upande wao mabondia waliofika katika mkutano huo miongoni mwa maoni na mapendekezo waliyotoa ni pamoja na:

  1. Mikataba halali ya pambano lolote lile ipitie katika kamati ya ngumi za kulipwa.
  2. Bondia kuambatana na watu wawili kwenda nje ya nchi katika pambano la ngumi kimataifa.

166 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/02/28/kamati-ya-ngumi-za-kulipwa-yakutana-na-mabondia-kupata-maoni-yao/">
RSS