BMT LATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA GWIJI WA SOKA ARTHUR MAMBETA

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akitoa pole juu ya msiba wa Arthur Mambeta
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akitoa pole juu ya msiba wa Arthur Mambeta

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Ndugu Mohammed Kiganja amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” na klabu ya wekundu wa msimbazi Simba Arthur Mambeta aliyefariki dunia Jumatano ya Tarehe 28 February 2018, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu.

Katika salamu hizo za rambirambi Katibu Kiganja amesema ni Pigo kubwa sana kumpoteza mchezaji huyo aliyelisaidia Taifa kwa hali na mali katika mchezo wa mpira wa miguu, na kutoa pole kwa familia,ndugu jamaa na marafiki.

Gwiji wa soka wa zamani wa klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars akiwa hospitali kuuguza maradhi ya saratani yaliyokuwa yakimsumbuwa kwa kwa muda mrefu katika enzi za uhai wake.
Gwiji wa soka wa zamani wa klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars akiwa hospitali kuuguza maradhi ya saratani yaliyokuwa yakimsumbuwa kwa kwa muda mrefu katika enzi za uhai wake.

“Ni masikitiko makubwa kumpoteza Mambeta ambaye alilitumikia Taifa naungana kumuombea marehemu na ninatoa pole kwa familia yake,wanafamilia wa mpira wa miguu, ndugu na jamaa pamoja na marafiki, Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya Marehemu Arhtur Mwambeta,Amina.

Mambeta alianza kuchezea Simba SC miaka ya 1960 enzi hizo ikiitwa Sunderland kama kiungo mshambuliaji hodari kuanzia klabu yake hadi timu ya taifa.

Kocha wa Tanzania miaka hiyo, Milan Celebic raia wa Yugoslavia alishawahi kukaririwa kuunda timu ya Taifa bila ya Arthur Mambeta ni sawa na kula chakula bila ya chumvi au chai iliyokisa sukari

Arthur Mambeta ndiye mchezaji pekee wa Tanzania aliyekuwemo kwenye kikosi cha kwanza cha kombaini ya Afrika Mashariki iliyocheza na West Bromwich Albion ya England mwaka 1974 Uwanja wa Nakivubo mjini Kampala, Uganda.

121 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/03/01/bmt-latuma-salamu-za-rambirambi-kifo-cha-gwiji-wa-soka-arthur-mambeta/">
RSS