WAVU WAWEKA WAZI MIKAKATI YAO 2018

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania Meja Generali Patrick Peter Mlowezi akielezea Dira ya chama chao, ni kuufanya mchezo wa wavu kuwa na nguvu, maarufu na unaopendwa na wadau wengi hapa nchini.pembeni kulia ni Mwenyekiti wa kamisheni ya wavu wa ufukweni, Shukuru Said.

Uongozi wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) umeweka wazi mikakati yao ya maendeleo ya mchezo huo kwa wadau wao kwa mwaka 2018 naya miaka minne (4) ya uongozi ulioko madarakani.

Mikakati hiyo imetolewa leo Machi 02, 2018 katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa  Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania Meja Generali Patrick Peter Mlowezi ameeleza kuwa, Dira ya chama chao ni kuufanya mchezo wa wavu kuwa na nguvu, maarufu na unaopendwa na wadau wengi hapa nchini na dhima yao kuupeleka mchezo huo machoni na masikioni mwa Watanzania wote ili uchezwe wakati wote.

“Dira yetu kuufanya mchezo huu kuwa na nguvu, maarufu na upendwe na watu wengi pamoja na kuupeleka machoni na masikioni mwa Watanzania wote ili uchezwe wakati wote,” alisema Mlowezi.

Hata hivyo Mlowezi alieleza kuwa, ili kufanikisha dira na dhima ya chama chao wamejiwekea malengo ili kuleta maendeleo ya mchezo huo nchini,  ikiwa ni pamoja na kuwa na Katiba bora, walimu, waamuzi mahiri na wakutosha.

Aliongeza kuwa, Uongozi wake umelenga kukuza mpira wa wavu na hasa wa ufukweni, kujenga viwanja, kuanzisha na kuendeleza vituo vya watoto pamoja kuanzisha mashindano ya vijana.

Malengo mengine ni kushiriki mashindano ya kikanda na kimataifa, kuwa na vitendea kazi vya mchezo, wapata wafadhili wa kudumu na chama kujitegemea.

Mwenyekiti wa kamisheni ya wavu wa ufukweni, Shukuru Said akifafanua kuhusu kalenda ya chama cha mpira wa Wavu ya mwaka 2018. kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania Meja Generali Patrick Peter Mlowezi

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kamisheni ya wavu wa ufukweni, Shukuru Said aliyefafanua kuhusu kalenda ya chama ya mwaka 2018, alisema moja ya tukio ni ufunguzi wa kalenda ya mwaka 2018 tukio litakalofanyika tarehe 3 Machi na kuhusisha michuano kati ya timu ya wanaume kutoka Faru na Makongo na Wanawake kutoka Makongo na Jeshi stars.

59 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/03/02/wavu-waweka-wazi-mikakati-yao-2018/">
RSS