JESHI STARS WASALIMU AMRI KWA MAKONGO KATIKA MCHEZO WA UFUNGUZI WA MSIMU TAVA.

Mmoja wa wachezaji wa Timu ya makongo aliyeruka juu kupiga mpira upande wa Jeshi stars na kupata pointi katika mchezo wa ufunguzi wa Msimu wa mashindano ya mpira wa Wavu chini ya TAVA.
Mmoja wa wachezaji wa Timu ya makongo aliyeruka juu kupiga mpira upande wa Jeshi stars na kupata pointi katika mchezo wa ufunguzi wa Msimu wa mashindano ya mpira wa Wavu chini ya TAVA.

Timu ya Jeshi ya mpira wa wavu Jeshi stars imekubali kipigo cha seti 3 – 2 kutoka kwa timu ya wanawake  ya shule ya sekondari ya makongo katika mchezo wa kufungua msimu wa mashindano ya mpira wa wavu chini ya chama cha mpira wa wavu Tanzania (TAVA) uliofanyika leo tarehe 3 Machi 2018, katika uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini Dar es salaam.

kikosi cha Timu ya mpira wa Wavu Jeshi Stars.
kikosi cha Timu ya mpira wa Wavu Jeshi Stars kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi dhidi ya timu ya makongo.

Mchezo huo umepigwa baada ya Uongozi wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) kuweka wazi mikakati yao ya maendeleo ya mchezo huo kwa wadau wao kwa mwaka 2018 naya miaka minne (4) ya uongozi ulioko madarakani.

kikosi cha Timu ya mpira wa Wavu ya Makongo wakiomba dua kabla ya mchezo wao dhidi ya Jeshi stars.
kikosi cha Timu ya mpira wa Wavu ya Makongo wakiomba dua kabla ya mchezo wao dhidi ya Jeshi stars.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kamisheni ya wavu wa ufukweni, Shukuru Said amesema mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya tukio katika kalenda ya chama ya mwaka 2018.

686 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/03/03/jeshi-stars-wasalimu-amri-kwa-makongo-katika-mchezo-wa-ufunguzi-wa-msimu-tava/">
RSS