UMISSETA NA UMITASHUMTA 2018 SASA RASMI KUFANYIKA MWANZA.

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Selemani Said Jafo(Mb) akitamka Rasmi kuwa Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA 2018 kufanyika Jijini Mwanza
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Selemani Said Jafo(Mb) akitamka Rasmi kuwa Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA 2018 kufanyika Jijini Mwanza.

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Selemani Said Jafo(Mb) leo hii tarehe 9 Machi 2018, amezindua rasmi Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) pamoja na Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yatakayofanyika Mkoani Mwanza mwezi Juni mwaka huu.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere- Chuo cha Mipango mjini Dodoma Mheshimiwa Jafo amesema ni muhimu kuienzi michezo ya UMISETA na UMITASHUMPTA kwani vijana wengi ambao wanashiriki katika michezo Shule za msingi na Sekondari, wana nafasi kubwa sana kufanya vizuri kitaaluma na kujitengenezea ajira nchini.

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Selemani Said Jafo(Mb) akiwasili katika Warsha ya Uzinduzi wa Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA 2018 Ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere- Chuo cha Mipango Mjini Dodoma.

“Ni vizuri na muhimu kuienzi Michezo ya UMISETA na UMITASHUMPTA kwani vijana wengi ambao wanashiriki katika michezo shule za msingi na sekondari wana nafasi kubwa sana kufanya vizuri kitaaluma na kujitengenezea ajira nchini,”Alisema Mh. Jafo.

Aidha Mheshimiwa Jafo amewaagiza maafisa wote wanaosimamia michezo mashuleni kuhakikisha kuwa vipindi vya michezo vinatendewa haki asilimia mia moja na vinatumika vizuri kimichezo, ili kuhakikisha kuwa shule zao zinafanya vizuri katika mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMPTA sanjari na kuhakikisha shule zinazosajiliwa katika Mashindano hayo ziwe na miundombinu mizuri kama vile Viwanja.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja akimsihii Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI kuliangalia upya suala la kufungwa kwa chuo cha ualimu BUTIMBA, kwani bado vizazi vijavyo vinahitaji waalimu wa elimu ya michezo mashuleni ambao  wapo kwa nadra sana nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja hayo amesema kuwepo kwa mashindano hayo ni muendelezo tu wa kazi nzuri zinazofanywa na waalimu wakisimamiwa na maafisa elimu wa mikoa na wilaya kutekeleza yale ambayo yameagizwa kwenye Wizara sanjari na kuendeleza pamoja na kujifunza uzalendo nchini.

“Mheshimiwa waziri kuwepo kwa mashindano haya ni muendelezo tu wa kazi nzuri zinazofanywa na waalimu mashuleni wakisimamiwa na maafisa elimu wa mikoa na wilaya kutekeleza yale ambayo yameagizwa kwenye Wizara sanjari na kuendeleza pamoja na kujifunza uzalendo nchini”Alisema Katibu Kiganja.

Aidha Katibu Kiganja amemuomba Mheshimiwa waziri kuliangalia upya suala la kufungwa kwa chuo cha ualimu BUTIMBA, kwani bado vizazi vijavyo vinahitaji waalimu wa elimu ya michezo mashuleni ambao  wapo kwa nadra sana nchini.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja akimkabidhi Mh. Jafo vitabu vya Aiba na Michezo vinavyoonyesha Shule za Msingi zinafundiha Michezo.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohammed Kiganja akimkabidhi Mh. Jafo vitabu vya Aiba na Michezo vinavyoonyesha Shule za Msingi zinafundiha Michezo.

Nae Meneja wa kampuni ya Vinywaji vya Coca Cola Tanzania Sialuizi Shayo, amemshukuru Mh. Jafo kwa kuwapa fursa ya kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Serikali kwa ujumla katika suala la kukuza vipaji vya michezo Tanzania na kutumaini kuwa mwaka huu mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA yatakuwa mazuri lakini pia kupunguza changamoto zilizowakabili katika mashindano yaliyopita kwani ndoto ya kampuni hiyo ni kugusa wanafunzi na vijana wengi kimichezo.

Meneja wa kampuni ya Vinywaji vya Coca Cola Tanzania Sialuizi Shayo, akimshukuru Mh. Jafo kwa kuwapa fursa ya kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Serikali kwa ujumla katika suala la kukuza vipaji vya michezo Tanzania

“Nakushukuru sana Mheshimiwa waziri kwa kutupa fursa ya kushirikiana na ofisi yako pamoja na serikali kiujumla katika suala la kukuza vipaji vya michezo Tanzania na matumaini yetu mwaka huu mashindano yatakuwa mazuri,lakini pia kupunguza changamoto zilizotukabili katika mashindano yaliyopita kwani ndoto ya kampuni yetu ni kugusa wanafunzi na vijana wengi kimichezo”Alisema Sialuizo.

1,983 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/03/09/umisseta-na-umitashumta-2018-sasa-rasmi-kufanyika-mwanza/">
RSS