DKT. MWAKYEMBE ASIKITISHWA NA KIFO CHA NGURI WA KIKAPU BI. YVONNE CHRISTOPHER.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) akielezea jinsi Taifa lilivyopata pigo kuondokewa na mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya wanawake (JKT Queens) Bi. Yvonne Christopher Wambura aliyefariki dunia tarehe 21 Machi, 2018 Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya wanawake (JKT Queens) Bi. Yvonne Christopher Wambura kilichotokea tarehe 21 Machi, 2018 Jijini Dar es salaam.

Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa sekta ya Michezo imepoteza mmoja wa wanamichezo mahiri na hodari aliyeitumikia timu yake kwa juhudi kubwa.

Waziri Mwakyembe ametoa pole kwa familia ya marehemu, uongozi wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), wachezaji wa timu ya JKT, ndugu, jamaa na wadau wote wa michezo nchini, na kuwaombea mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Wakati wa uhai wake marehemu Bi. Yvonne alikuwa mchezaji wa timu ya wanawake (JKT Queens) na magereza zinazoshiriki ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam.

142 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/03/23/dkt-mwakyembe-asikitishwa-na-kifo-cha-nguri-wa-kikapu-bi-yvonne-christopher/">
RSS