MPIRA WA MAGONGO KUPATA VIONGOZI WAPYA MEI 6, 2018.

Wachezaji wa mchezo wa mpira wa magongo wakiwa katika mazoezi uwanja Lugalo Jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa mchezo wa mpira wa magongo wakiwa katika mazoezi uwanja Lugalo Jijini Dar es salaam.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza uchaguzi wa chama cha mpira wa magongo unatarajiwa kufanyika Tarehe 6 Mei, 2018 mkoani Tanga.

Akitangaza uchaguzi huo mbele ya waandishi wa habari leo hii  Machi 23, 2018, katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari amesema fomu zitaanza kutolewa katika ofisi za Baraza zilizopo uwanja wa Taifa, na pia kupatikana katika tovuti ya Baraza ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz, kuanzia tarehe 26 Machi hadi 25 Aprili mwaka 2018.

Aidha Afisa Najaha amesema usaili utafanyika siku hiyo ya uchaguzi asubuhi, halafu utafuatiwa na mkutano mkuu kasha uchaguzi wenyewe.

Nafasi zinazogombewa ni;

      NAFASI                                                                              ADA

  1. Mwenyekiti                                                              100,000/=
  2. Makamu Mwenyekiti                                             100,000/=
  3. Katibu Mkuu                                                            100,000/=
  4. Katibu Mkuu msaidizi                                            100,000/=
  5. Mweka Hazina                                                         100,000/=
  6. Wajumbe                                                                    50,000/=

Kwa upande wa sifa za wagombea ambao watajitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, Afisa Najaha amesema kiongozi lazima awe na sifa zifuatazo:

  1. Awe ni Raia wa Tanzania
  2. Awe na uzoefu wa uongozi pamoja na taaluma za uongozi wa Michezo.
  3. Awe na ujuzi wa mchezo wa Mpira wa Magongo.
  4. Awe hajatenda kosa lolote la Jinai.

Hivyo basi kutoa wito kwa wadau wote wenye sifa na wenye nia njema ya kuendeleza mchezo wa mpira wa magongo nchini kujitokeza kwa wingi kuchukuwa fomu, ili waweze kupatikana viongozi bora.

 

196 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/03/23/mpira-wa-magongo-kupata-viongozi-wapya-mei-6-2018/">
RSS